Mabalozi
wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nje ya Nchi
wameelekezwa kujipanga, kushiriki na kutafuta fursa zitakazowezesha
bidhaa mbalimbali za Tanzania kupata masoko ya uhakika katika nchi
walizopo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi wakati
akizungumza na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na kuongeza
kuwa , Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatamka bayana juu ya diplomasia
ya uchumi sambamba na kuimarisha sauti ya Tanzania na taswira yake
katika medani ya uhusiano wa kikanda na kimataifa.
Prof. Kabudi
ameongeza kuwa ili kufanikisha hilo Balozi zinapaswa kuimarisha ushiriki
wa Tanzania katika jumuiya nyingine za kimataifa zikiwemo, Indian Ocean
Rim Association, Indian Ocean Tuna Commission, South South Commission,
South West Indian Ocean Fisheries Commission.
Aidha amewataka
Mabalozi hao kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoyatoa wakati
akizundua Baraza la Wawakilishi ya kutaka Uchumi wa Bluu kupitia uvuvi
wa Bahari Kuu unakuwa na manufaa kwa Wananchi hususani katika kuongeza
mapato, ajira na kukuza uchumi kwa kuzingatia kuwa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni ya Muungano.
Pia Prof.
Kabudi amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na
Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika maendeleo ya Taifa na
kuzielekeza Balozi zianze na ziboreshe kanzi data ya Diapora ikiwa ni
pamoja na kuwahimiza kuanzisha Jumuiya zao.
“Natambua kazi hiyo
inaendelea na kwa sasa tuna data za diaspora takriban 98,658 na kuna
jumuiya 77 za diaspora. Nichukue fursa kusisitiza umuhimu wa Balozi zetu
kuboresha na kuharakisha zoezi hili kwa kubuni njia mbalimbali za
kuwaandikisha”. Amesema Prof. Kabudi
Mkutano huo wa Prof.
Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi umehudhuriwa
pia na Naibu Waziri, Mhe William Tate Ole Nasha, Katibu Mkuu Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Home
KIMATAIFA
Kitaifa
Mabalozi Wanaoiwakilisha Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Nje Ya Nchi Wahimizwa Kuongeza Juhudi Za Kufuta Masoko
Post A Comment: