Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Izack Amani akisaini kitabu cha msombolezo kilichopo katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Meneja msaidizi wa Benki ya Azania Tawi la Arusha,Yusufu Lenga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofika kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Afisa mahusiano wa Benki ya Azania Tawi la Arusha,John Machota akieleza namna ambavyo atamkumbuka hayati Dkt.John Magufuli katika masuala mazima ya kimaendeleo.
Na Jusline Marco-Arusha
Askofu
wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha,Izack Amani amesema kuwa watamkumbuka na
kumuenzi hayati Dkt.John Magufuli kupitia kazi alizozifanya kwa
watanzania kwa vile alivyokuwa jasiri na mwenye kuthubutu katika uletaji
wa maendeleo na kufungua ukurasa mpya kwa watanzania.
Akisaini
kitabu cha Maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Askofu
Amani amesema kupitia yale aliyoyafanya hayati Dkt.Magufuli watanzania
wanapaswa kujifunza kufanya kazi kwa uaminifu wakati wakiwa na muda huku
wakiomba neema ya kutumia muda huo vizuri na kuchangia vipaji vyao kwa
ukarimu kwa maendeleo ya nchi.
"Hayati Dkt.Magufuli
alifungua ukurasa mpya kwa Tanzania na kuandika historia mpya,mabadiliko
makubwa ya ujasiri na uthubutu na kuona kwamba kila kikundi kinashiriki
furaha ya uhuru."Alieleza Askofu Amani
Pamoja na hayo Askofu
Amani amewataka watanzania kutambua kuwa Mungu amemuumba mwanadamu kwa
malengo na kuweka ndani tamaa ya maendeleo na kuwapatia vipaji na karama
mbalimbali hivyo wanapaswa kuendelea kumshuru Mungu kwa yote
waliyojaliwa na kuwa na roho ya ushirikiano kuanzia ngazi ya
famili,jamii na taifa kwa ujumla.
"Tujifunze kwa hayati
Dkt.Magufuli kuwa alikuwa na nia njema na amejitolea kwa ajili ya
kusaidia watu wote kwa tabaka tofauti tofauti,ule ukarimu wa kumrudishia
shukurani kupitia kuwatumikia watu kwa upendo na uaminifu huku
tukiepuka utoaji na upokeaji wa rushwa."Alisisitiza Askofu Amani
Katika
hatua nyingine Uongozi wa Banki ya Azania Tawi la Arusha umeazimia
kumuenzi hayati Dkt.Magufuli kwa kile alichokifanya enzi ya uhai wake
ikiwemo uanzishwaji wa mahakama ya mafisadi
Akitoa pole kwa
watanzania na familia ya hayati Dkt.John Magufuli,Meneja msaidizi wa
Benki ya Azania Tawi la Arusha,Yusufu Lenga amesema kuwa kama taasisi ya
fedha watamkumbuka hayati Dkt.Magufuli kwa uanzishwaji wa mahakama za
mafisadi na kusaidia watu kuwa na nidhamu ya fedha.
"Kupitia
mahakama ya mafisadi iliyoanzishwa na hayati Dkt.Magufuli kila mtu
ameona jukumu lake ni kutafuta fedha halali na kuyafanya maisha ya
kibiashara yawe ni maisha ambayo mtu ayafanyi kwa njia za mkato."alisema
Lenga
Amesema kutokana na hilo,imesaidia watu wa taasisi ya
fedha kutokuwa na fedha nyingi za mashaka lakini pia wanaendelea kukagua
kila fedha ambayo huingia kwenye taasisi ambapo asilimia kubwa nidhamu
ya wafanyabiashara,wafanyakazi na wengine kwenye sekta ya kifedha
imekuwa ya hali ya juu.
Kwa upande wake Afisa mahusiano wa Benki
hiyo,John Machota amesema kywa kama taasisi ya fedha ya Azania
wataendelea kumkumbuka hayati Dkt.Magufuli kwa kuifanya heshima iwepo
serikalini pamoja na utolewaji wa elimu bure ambayo imefanya kila mtoto
anapata elimu hiyo pasipo kubugudhiwa.
"Taarifa za kifo cha
Mhe.Rais zilinikosesha usingizi kwasababu niliangalia mambo ambayo
ameyafanya na kuyaanzisha katika nchi yetu niliwaza yataendelezwa vipi
kweli sikupata usingizi."alieleza Machota
Amebainisha kuwa
watamuenzi hayati Dkt.Magufuli kupitia fursa ya kuwapatia elimu bure
watanzania ambapo amewataka watanzania kuwa na umoja pamoja na
mshikamano katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Mhe.Samia Siluhu
na kuamini kuwa ataweza kuwafikisha watanzania kule ambapo hayati
Dkt.Magufuli angeweza kuwafikisha.
Post A Comment: