Mfanyabiashara
wa Duka la Chakula, Mama Mary (kulia) akionesha cheti chake cha usajili
wa duka la chakula wakati maafisa wa TBS wakitoa elimu ya usajili wa
majengo ya chakula na vipodozi kwa wafanyabiashara waliopo soko kuu na
stendi kuu ya mabasi wilayani Musoma.
Afisa
udhibiti ubora,Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS),akiwaasa
wafanyabiashara Musoma waliopo katika soko la Nyasho mlango mmoja
kutokuuza nguo za ndani za mitumba kwani haziruhusiwi ili kuepuka hasara
na kuwahimiza waliopo Nyasho soko kuu kusajili majengo ya chakula na
vipodozi
Wanafunzi
wa shule ya msingi Mwisenge A wilayani Musoma wakipatiwa elimu ya
viwango itakayowasaidia kuwa mabolozi wazuri wa masuala ya ubora.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Mwisenge A wilayani Musoma wakipatiwa elimu ya
viwango itakayowasaidia kuwa mabolozi wazuri wa masuala ya ubora.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya viwango vya ubora wa bidhaa katika wilaya ya Musoma ambapo imeweza kukutana na Wafanyabiashara mbalimbali pamoja na wanafunzi na kuwahimiza kutumia bidhaa zenye ubora ili kuweza kumlinda mlaji.
Akizungumza mara baada ya kutembelewa na maafisa wa TBS ofisini kwake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mjini, Bi.Fidelica Myovella ameipongeza TBS kwa kutoa elimu kwa wananchi katika ngazi ya Wilaya.
"Elimu hii mnayoitoa TBS itaongeza ufahamu na kuhakikisha suala la uuzaji wa bidhaa hafifu sokoni linapungua kama sio kwisha kabisa". Alisema Bi.Fidelica.
Pamoja na hayo TBS imetoa elimu ya viwango pia kwa wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma, Mwisenge pamoja Bweri wilayani humo ambapo muitikio wa uelewa wa elimu hiyo ni kubwa.
Post A Comment: