Baada
ya kushuhudia Mwili wa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amelala,Sasa
nimeamini Jabali lenye Moyo wa Simba na akili ya Duma amelala Usingizi
wa Mauti.
Usiku ule wa tarehe 17 Machi, ni usiku Mgumu kuwahi
kutokea katika Maisha yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye
huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku
zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia
zaidi matokeo ya kazi aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya
pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.
Kuondoka kwake kwa
wakati huu kuliniingiza Ganzi nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama
Janeth amempoteza Mume, Taifa limempoteza Baba na Rais, Africa
Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu imempokea shujaa wa
Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia,
akailinda imani kwa kulitambulisha jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa,
Na sasa amemaliza mwendo na amepumzika Miguuni kwa bwana wa vita.
MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.
Nenda
Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa
wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli
umeandika Dibaji mpya.
Hadithi
za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu
umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala
Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako
na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila
kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika
ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno
yetu.
Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana Mwenyewe.
Imenyamaza
sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi
wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza
shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala
Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.
Umetufunza
ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za
kufanya kwa ajili ya Taifa na vizazi tutakavyoviacha.Vilio vya wanyonge
na wasio na sauti vimefika kwenye kiti cha Enzi. Rest in power John,
Tutakutana Baadae.Bado ni salama Rohoni mwangu.
Nenda Baba, nyuma
yako kila tukitaka kulia tunakumbuka umetuachia Mama Samia. Kila
tukitaka kukata Tamaa tunamwona mama akiwa jasiri na kutupa tumaini
jipya la Mapambano.
Tanzania inakulilia pumzika kwa amani Jembe.
Ole Sabaya.
Post A Comment: