Jeneza lililobeba Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk.John Pombe Magufuli likiwasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa mwili huo.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na viongozi wastaafu wa Serikali zilizopita wamefika Uwanja wa Uhuru kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk.John Pombe Magufuli.
Dkt.Magufuli ambaye amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mnzena mkoani Dar es Salaam ambako alikuwa anapatiwa matibabu kutoka na maradhi ya moyo katika mfumo wa umeme , wananchi wa Dar es Salaam wakiongozwa na maelfu ya wananchi wamepata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Dkt.Magufuli.
DAWASA inaungana na watanzania wote kuombeleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk.John Pombe Magufuli Jeneza la lililobeba Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli likiwasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam leo March 20,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam leo Machi 20,2021.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) wakiwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kea ajili ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Post A Comment: