BODI ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mej.Gen(Mstaafu) Hamisi Semfuko imetembelea Pori la Akiba la Mapanga /Kipengere lililopo katika Mkoa wa Njombe na Mbeya na kufanya kikao na watumishi wa pori hilo.
Katika Safari hiyo Mwenyekiti wa Bodi aliambatana na Menejimenti ya TAWA ikiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Bw. Mabula Nyanda Misungwi pamoja na Naibu Kamishna wa Huduma za Utalii na Biashara Bw. Imani Nkuwi na uongozi wa Pori hilo uliongozwa na Meneja wa Pori Bw.Joas Makwati.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Mej.Gen (Mstaafu) Hamisi Semfuko akiongea wa watumishi wa Poria Akiba Mpanga/Kipengere aliwaelezea kuwa Lengo la safari yake na wajumbe wa Bodi ni kufanya ukaguzi wa uendelezaji miradi ya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya utalii na ufuatiliaji wa utelelezaji kazi.
Ameongeza kuwa Lengo ikiwa ni kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, kuongeza watalii na mapato na kuboresha utendaji wa Shirika.
Meneja wa Pori hilo Joas Makwati,alimueleza Mwenyekiti na msafara wake kuwa kuna, vivutio vya utalii, kwa Kuwepo kwa aina mbalimbali za Wanyamapori pia kuna maporomoko 7 ya maji ikiwemo Kimani ambayo ni maarufu, ya kuvutia na ya kipekee katika ukandaa wa kusini mwa Tanzania.
Aidha pia Ukanda wa maua na nyasi na miinuko na mabonde yanaifanya Hifadhi hiyo kuwa na mandhari nzuri.
Hata hivyo meneja huyo alimweleza Mwenyekiti wa Bodi kuwa Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosabisha kutofikiwa malengo mahususi ya kuanzishwa Kwake ikiwemo,upungufu wa watumishi na Ukosefu wa kambi za kitalii na barabara za kuvifikia vivutio.
kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi aliwakumbusha watumishi kufanya kazi kwa nidhamu, weledi, uadilifu na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
Pia amesema kuwa amefurahishwa na mawazo chanya yaliyowasilishwa Kwame yenye lengo la kuijenga Taasisi na kuifanya ipige hatua na hivyo kuwahakikishia kuwa maoni yao yamepokelewa na yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuleta tija kwa Shirika akishirikiana na Menajimenti ya TAWA.
Baada ya kikao hicho Mwenyekiti na msafara wake wakitembelea Maporomoko ya maji ya Kimani ambayo ni maarufu kutokana na maji yake kuanguka katika umbo la ngazi ngazi kwa umbali wa mita zaidi ya 70 na yanapoanguka ya natengeneza mvuke
Pia baada ya kuona Maporomoko ya maji ya Kimani alihitimisha safari yake Kwa kutembelea pango la Mtemi Mkwawa.
Pango hili linasadikiwa kutumiwa na Mtemi Mkwawa Kwa ajili ya mapumziko/Maficho kipindi cha vita ya wahehe na wajerumani.Pango lipo jirani na Maporomoko ya maji ya mto Kimani
Post A Comment: