WAZIRI wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema Kitabu cha Lugha ya Kiswahili cha Historia nchini kitaanza kitumika Machi 31 mwaka huu
WAZIRI Ndalichako aliyasema hayo Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa elimu kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu maudhui ya somo LA Historia Tanzania
Ndalichako alisema kuanza kwa kitabu hicho ni agizo la Rais John Magufuli ambalo alilitoa kwamba nchi yetu ili uwe
Mzalendo wa kweli lazima ujue Historia ya nchi yetu.
"Kitabu cha Historia cha kiswahili kitanaanza kutumika Machi 31 Mwaka huu kuanzia shule za awali ,Shule za msingi sekondari mpaka kidato cha sita " alisema Ndalichako.
Alisema kwa sasa Wizara inaanda rasimu ya vitabu hivyo Watanzania waweze kujua Historia ya nchi yao.
Dhumuni la kufundisha histoaria kwa ludha ya Taifa ni kujenga moyo wa uzalendo jamii iweze kujua Historia ya nchi yao .
Mkutano huo ulishirikisha wadau wa elimu kwa ajili ya kupokea maoni ambapo pia uliwashirikisha Machifu kutoa mikoa yote hapa nchini.
Alisema watapokea maoni na kuyafanyia kazi ili somo la Historia liwe na mvuto katika nchi yetu katika kuunga juhudi za Rais John Magufuli kukuza lugha hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tasisi ya Elimu Tanzania. Aneth Komba alisema Taasisi ya Elimu Tanzania imekamilisha kazi ya uandishi wa Rasimu za Mihtasari ya darasa la kwanza hadi la saba kidato cha kwanza mpaka cha NNE na kidato cha tano hadi cha sita.
Komba alisema katika taratibu za uandishi wa nyaraka hatua moja wapo kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu na watekelezaji wa mwisho wa mtaala pamoja na wasimamizi wa utekelezaji wa mtaala kwa lengo la kupata maoni yao juu ya utoshelevu wa mada na
Usahihi wa mbinu zinazotumika kufundisha na kujifunzia .
Alisema mkutano huo umewashirikisha vyuo vikuu,vyuo vya ualimu ,umoja wa machifu Tanzania ,chama cha Historia nchini,Wizara ya habari na Utamaduni,wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia,Ofisi ya Rais TAMISEMI,Bakwata na Christian social Service ,TAPIE,TAMUNGOSCO ,REDEOA ,TAPSHA .
Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania Chifu Masagati Fundikalisema alisema yeye na machifu wezake wa hapa nchini wapo tayari kufundisha somo hilo ikiwemo kusimamia mila na desturi kwa kushirikiana na serikali kwa dhumuni la kizazi kipya na jamii wafahamu Historia ya nchi yao.
Post A Comment: