Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo


 Na Scolastica Msewa, Kibaha.


Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linawashikiria watu wanne kwa kueneza uvumi na kutia hofu wananchi kwa kudai vifo vya watu wamekufa kwa corona.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini kibaha Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linawashikiria watu wanne hao waliokamatwa tangu tarehe 18 na 19 mwezi huu ndani ya mkoa wa Pwani kwa kutumia  mitandao ya kijamii kueneza uvumi na kutia hofu wananchi.

Kamanda Wankyo amesema Watuhumiwa hao na wengine wanaendelea kuwatafuta wanasambaza taarifa za uvumi za vifo vya watu wakidai wamekufa na corona.

Amesema watu hao wanataja na kupendekeza majina ya viongozi wa serikali waliotamani wafe haraka kwa corona.

"Pia wanatia watu hofu kubwa kwa kutumia mitandao hiyo ya kijamii kuwa Watanzania wengi watakufa kwasababu serikali haichukui tafadhali dhidi ya wananchi wake" alisema Wankyo.

Aidha Kamanda Wankyo amewataka Watuhumiwa hao kuwa ni Frank Almatia Nyange (47) mchaga fundi ujenzi na mkazi wa kongowe, Mosses Godluck Mgao(34) mhehe mfanyabiashara mkazi wa kongowe, Mohammed abdallah Lutambi mfanyabiashara mkazi wa mailmoja tangini, Bumija Mosses Senkondo (55) Mpare mjasiliamali mkazi wa mkuza.

Hatahivyo Kamanda huyo wa Polisi mkoa wa Pwani ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tafadhali ya ugonjwa wa corona na kufuata maelekezo yanayotolewa na wizara ya afya.

Share To:

Post A Comment: