*Baba Watoto waweka vituo vya kufikia katika kujua Maendeleo
*Sera za Ulinzi zatakiwa kuwekwa kwa kundi hilo
Na Chalila Kibuda
SHIRIKA la Kimatafa la Children Railway Africa kwa Kushirikiana na Baba Watoto limesema kuwa Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hawana uangalizi na kufanya watoto haki kukosa haki nyingi za msingi.
Watoto wa mitaani moja ya haki wanayoikosa afya kutokana na hakuna mtu wa kuweza kuwatowafatilia kwa karibu na hata majanga ya magonjwa ikiwemo la Corona hakuna mtu anayejua watoto hao wanaishije.
Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Habari wa Railway Children Africa Henry Mazunda amesema kuwa watoto hao sehemu sahihi ya kuishi ni nyumbani kwao au katika familia zao lakini wametoka kutokana na changamoto mbalimbali hivyo serikali inatakiwa kuweka sera ya ulinzi wa watoto hao.
Mazunda amesema katika mradi waliofanya kwa kushirikiana na Baba Watoto wameanzisha vituo vya kufikia watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani ambapo wanaweza kufua nguo, wakapata chakula na hadi matibabu lakini vituo hivyo sio vituo vya kudumu kwao kuishi.
Aidha amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani licha ya kuwa na sehemu ya kufikia wanachowashauri watoto ni pamoja na watoto kuwaunganisha na familia zao na kuwafatilia kwa karibu.
Mratibu wa Mlinzi wa Watoto wa Baba Watoto Tony Mafiye amesema watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wakiwa katika sehemu ya kufikia 'Dropping Center' wamekuwa ni watoto ambao wanajitambua kutokana na mifumo iliyopo katika usimamizi w masuala ya watoto.
Amesema kuwa watoto hao hata wakiwa mtaani asiponekana wanajua jinsi ya kufatilia na hata kama wamekamatwa wanakwenda kutoa dhamana pamoja na kutoa msaada wa kisheria.
Nae Afisa Mawasiliano na Utetezi wa Baba Watoto Brenda Mlwele amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wakiwa katika vituo vya kufikia wanajifunza vitu mbalimbali ikiwa ni kuwafanya wajisikie jamii inawajali.
Afisa Saikolojia Asha Salum amesema anapokutana na watoto anaongea nao kuangalia namna alivyoathirika kisaikolojia na kutoa ushauri wa kuwajenga upya.
Mwalimu wa Sanaa wa Baba Watoto Adam Famba amesema kuwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wanavipaji lakini hata watu hawajui lakini baadhi yao wanaweza kuimba.
Afisa wa Familia wa Baba Efransia Kisweka amesema kuwa watoto wangine wamewaunganisha na familia zao ambapo wanaendelea vizuri ikiwa pamoja wengine kwenda katika Mafunzo ya ufundi.
Mmoja wa Mama wa Mwenye mtoto aliyetoroka nyumbani Mwanaid Salum amesema anaishukuru Baba Watoto kwa kumuunganisha mtoto wake pamoja na kumjenga kisaikolojia ya kuishi.
Amesema tatizo la mtoto wake lilitokana na familia kumsema kutokana na mtoto huyo alizaliwa nje ya baba ambaye ameolewa na kusema kuwa hata husika katika urithi.
Amesema mtoto huyo anaendelea vizuri lakini hata ndugu wameacha kumsema.
Post A Comment: