Na HERI SHAABAN
SERIKALI imesema inatarajia kupeleka fedha kwa ajili ya sekta ya elimu Shule ya Msingi Maalifa Iliyopo Gongolamoto Wilayani Ilala yenye wanafunzi wa kawaida na wa mahitaji Maalum.
Hayo yalisemwa Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako katika ziara yake Mkoa Dar es Salaam Leo.
Profesa Ndalichako aliyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea Shule zenye Wanafunzi wa mahitaji maalum ili kujua changamoto zake .
"Mwezi Machi mwaka huu nitaelekeza fedha katika Shule ya maalifa ili liweze kujengwa jengo la Utawala LA Walimu awamu ya pili nitatoa fedha za kujenga Bwalo kwa ajili ya Shule hii " alisema Ndalichako.
Alisema kazi ya Walimu ni wito na Walimu wanajituma katika utoaji wa Elimu kwa ajili ya kuwafundisha Watoto
Amewataka Walimu kufanya kazi kwa weledi ili kukuza sekta ya Elimu na kukuza taaluma Taifa lolote linaitaji watu wake wasome ili kuweza kupata viongozi wa baadae .
Wakati huohuo alisema SERIKALI imejipanga vizuri kuwalipa walimu Wastaafu mafao yao mara baada kustaafu kufundisha .
Joyce Ndalichako alisema SERIKALI imeweka mikakati yake vizuri kuakikisha Walimu wote wanalipwa mafao yao kwa wakati .
"Naagiza Walimu wote mara baada kustaafu fatilia nyaraka zako vizuri ili serikali iweze kuwalipa kwa wakati " alisema Ndalichako.
Ndalichako alipongeza shamba darasa Shule ya Msingi Maalifa Wilayani Ilala inajikwamua kiuchumi ambapo wanajifunza Watu Wazima ,ambapo aliagiza Shule zote nchini kuwa na kituo cha Elimu ya Watu Wazima .
Ametoa wito nchini kuanzishwa kwa vituo hivyo watu waweze kuelimika katika kukuza Elimu hiyo.
Katika hatua nyingine ameagiza Watumishi kumi Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambao wanashughulika kutengeza vitabu vya Wanafunzi wa mahitaji Maalum kurejea nyumbani hapo uzalizashaji wa vitabu utakapoanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija amesema Shule za serikali wilaya ya Ilala kwa sasa ufaulu wake upo juu na Wazazi wanapeleka watoto Shule hizo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amempongeza Rais John Magufuli kwa kuelekeza fedha nyingi katika sekta Elimu ILALA.
Mwisho
Post A Comment: