‌Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akifungua kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma, katikati ni Naibu wake, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (katikati) akizungumza katika kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wake Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula akizungumza katika kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma, Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Naibu wake Mhe. Mhandisi Kundo Mathew.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akizungumza na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Hassan Mwang’ombe (kulia) baada ya kufungua kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika hilo jijini Dodoma, Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi akisikiliza na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula.

Baadhi ya mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania wakimsikiliza Waziri wa wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akifungua rasmi kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) jijini Dodoma.

……………………………………………………………………..
Na‌ ‌Faraja‌ ‌Mpina‌ ‌–‌ ‌WMTH‌ 
 
Waziri‌ ‌wa‌ ‌Mawasiliano‌ ‌na‌ ‌Teknolojia‌ ‌ya‌ ‌Habari‌ ‌Mhe.‌ ‌Dkt.‌ ‌Faustine‌ ‌Ndugulile‌ ‌ameliagiza‌ 
Shirika‌ ‌la‌ ‌Posta‌ ‌Tanzania‌ ‌(TPC)‌ ‌kuangalia‌ ‌upya‌ ‌muundo‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌kurugenzi‌ zake‌ ‌kama‌ ‌vimekaa‌ ‌sawa‌ ‌na‌ ‌kukidhi‌ ‌mahitaji‌ ‌kwa‌ ‌lengo‌ ‌la‌ ‌kuongeza‌ ‌tija,‌ ‌ufanisi‌ ‌na‌ ‌utendaji‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌hilo.‌ 
 
Dkt.‌ ‌Ndugulile‌ ‌amezungumza‌ ‌hayo‌ ‌alipokuwa‌ ‌akifungua‌ ‌kikao‌ ‌kazi‌ ‌cha‌ ‌Menejimenti‌ ‌na‌ 
Mameneja‌ ‌wa‌ ‌Mikoa‌ ‌yote‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌la‌ ‌Posta‌ ‌Tanzania‌ ‌kinachofanyika‌ ‌kwa‌ ‌siku‌ ‌tatu‌ ‌jijini‌ 
Dodoma‌ ‌ili‌ ‌kujadili‌ ‌utekelezaji‌ ‌wa‌ ‌majukumu‌ ‌ya‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌katika‌ ‌ngazi‌ ‌ya‌ ‌Mikoa.‌ 
 
“Mkaangalie‌ ‌upya‌ ‌mgawanyo‌ ‌wa‌ ‌majukumu‌ ‌yenu‌ ‌ili‌ ‌yale‌ ‌yanayoweza‌ ‌kufanyika‌ ‌katika‌ ‌ngazi‌ ya‌ ‌mkoa‌ ‌yafanyike‌ ‌mkoani‌ ‌na‌ ‌yale‌ ‌ya‌ ‌Makao‌ ‌Makuu‌ ‌yafanyikie‌ ‌Makao‌ ‌Makuu,‌ ‌nchi‌ ‌hii‌ ‌ina‌ ‌mikoa‌ ‌31‌ ‌jipangeni‌ ‌vizuri‌ ‌kuhakikisha‌ ‌uwepo‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌katika‌ ‌kila‌ ‌Mkoa”,‌ ‌Dkt.‌ ‌Ndugulile‌ 
 
Aidha,‌ ‌amezungumzia‌ ‌Sera‌ ‌ya‌ ‌Posta‌ ‌kuwa‌ ‌ni‌ ‌ya‌ ‌zamani‌ ‌na‌ ‌Sheria‌ ‌yake‌ ‌sio‌ ‌Rafiki‌ ‌sana‌ 
kuwezesha‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌kufikia‌ ‌maono‌ ‌yake‌ ‌na‌ ‌maono‌ ‌ya‌ ‌Wizara.‌ 
 
Amesema‌ ‌kuwa‌ ‌Wizara‌ ‌imefanya‌ ‌mabadiliko‌ ‌madogo‌ ‌ya‌ ‌Sheria‌ ‌ya‌ ‌Posta‌ ‌ili‌ ‌kuongeza‌ ‌ufanisi‌ katika‌ ‌utendaji‌ ‌na‌ ‌kusisitiza‌ ‌ni‌ ‌vema‌ ‌kutumia‌ ‌fursa‌ ‌ya‌ ‌kikao‌ ‌kazi‌ ‌hicho‌ ‌kukusanya‌ ‌maoni ‌ya‌ ‌Sera‌ ‌mpya‌ ‌ya‌ ‌posta‌ ‌inayoenda‌ ‌kutengenezwa‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌mabadiliko‌ ‌ya‌ ‌sheria‌ 
yanayotarajiwa.‌ 
 
“Shirika‌ ‌ndio‌ ‌mtekelezaji‌ ‌wa‌ ‌Sera‌ ‌ambazo‌ ‌Wizara‌ ‌inaandaa‌ ‌hivyo‌ ‌ni‌ ‌vema‌ ‌Mameneja‌ 
wakahusishwa‌ ‌ili‌ ‌nao‌ ‌watoe‌ ‌maoni‌ ‌yao‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌kuangalia‌ ‌namna‌ ‌ya‌ ‌kujipanga‌ ‌katika‌ 
utekelezaji‌ ‌wa‌ ‌mipango‌ ‌yao‌ ‌wanayotarajia‌ ‌kuifanya”,‌ ‌Dkt.‌ ‌Ndugulile‌ 
 
Naye‌ ‌Naibu‌ ‌Waziri‌ ‌wake‌ ‌Mhe.‌ ‌Mhandisi‌ ‌Kundo‌ ‌Mathew‌ ‌amelitaka‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌kujitangaza‌ 
zaidi‌ ‌ili‌ ‌kukuza‌ ‌biashara‌ ‌za‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌kwa‌ ‌kuanzia‌ ‌ndani‌ ‌ya‌ ‌Shirika‌ ‌kwa‌ ‌kutumia‌ ‌mbinu‌ 
mbalimbali‌ ‌za‌ ‌kutangaza‌ ‌masoko‌ ‌pamoja‌ ‌na‌ ‌kutengeneza‌ ‌vifaa‌ ‌vyenye‌ ‌nembo‌ ‌ya‌ ‌posta‌ 
mfano‌ ‌kutengeneza‌ ‌na‌ ‌kutumia‌ ‌shajara‌ ‌zenye‌ ‌nembo‌ ‌ya‌ ‌Shirika‌ ‌hilo.‌ 
 
Kwa‌ ‌upande‌ ‌wa‌ ‌Katibu‌ ‌Mkuu‌ ‌wa‌ ‌Wizara‌ ‌hiyo‌ ‌Dkt.‌ ‌Zainab‌ ‌Chaula‌ ‌ametoa‌ ‌angalizo‌ ‌kwa‌ 
watendaji‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌hilo‌ ‌wanaokaimu‌ ‌nafasi‌ ‌za‌ ‌uongozi‌ ‌kuwa‌ ‌hawatoweza‌ ‌kuthibitishwa‌ 
katika‌ ‌nafasi‌ ‌wanazokaimu‌ ‌kama‌ ‌hawatofanya‌ ‌kazi‌ ‌vizuri‌ ‌zaidi‌ ‌kwa‌ ‌kujituma‌ ‌ili‌ ‌kuonesha‌ 
wanastahili‌ ‌kupanda‌ ‌na‌ ‌kuthibitishwa.‌ 
 
Naibu‌ ‌Katibu‌ ‌Mkuu‌ ‌wa‌ ‌Wizara‌ ‌hiyo‌ ‌Dkt‌ ‌Jim‌ ‌Yonazi‌ ‌amewazungumzia‌ ‌watendaji‌ ‌wa‌ ‌Shirika‌ ‌la‌ 
Posta‌ ‌kuwa‌ ‌ni‌ ‌wasikivu‌ ‌na‌ ‌wapo‌ ‌tayari‌ ‌kubadilika,‌ ‌kuanzia‌ ‌mameneja‌ ‌mpaka‌ ‌Posta‌ ‌masta‌ 
Mkuu‌ ‌hivyo‌ ‌ni‌ ‌rahisi‌ ‌kufanya‌ ‌nao‌ ‌kazi‌ ‌kwa‌ ‌sababu‌ ‌wanapokea‌ ‌maelekezo‌ ‌na‌ ‌kuyafanyia‌ ‌kazi.‌ 
 
 
Imetolewa‌ ‌na‌ ‌Kitengo‌ ‌cha‌ ‌Mawasiliano‌ ‌Serikalini‌ 
Wizara‌ ‌ya‌ ‌Mawasiliano‌ ‌na‌ ‌Teknolojia‌ ‌ya‌ ‌Habari‌
Share To:

Post A Comment: