Naibu Waziri Kilimo Mhe. Hussein Bashe leo mchana tarehe 17 Februari, 2021 amesema msaada wa Euro milioni 100 kutoka (Umoja wa Ulaya – European Union) zitatumika sawa sawa na mahitaji ya nchi kwenye kukuza na kuendeleza Sekta ya Kilimo hususan eneo la ujenzi wa miundombinu ya barabara zinatotumiwa na Wakulima wa chai pamoja na kuanzisha soko (Mnada) chai Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Bashe amesema kiasi cha Euro milioni 100 kutoka Umoja wa Ulaya zitakwenda moja kwa moja kwenye maeneo ya kukuza na kuendeleza Sekta ya Kilimo na kuongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kitatolewa katika kipindi cha miaka minne ambapo kila mwaka fedha zitakazotolewa ni sawa na Euro milioni 25.
Naibu Waziri Bashe ameyataja maeneo ya kipaumbele kwenye Sekta ya kilimo ambayo kiasi cha Euro milioni 100 ambazo zitatumika ni pamoja na ujenzi wa miundombinu (Barabara za vijijini kutoka kwenye mashamba ya chai kwenda kwenye viwanda vya chai; Ujenzi wa Kituo maalum cha kuhifadhia mazao ya kilimo (Kurasini Integrated Agro-Hub) kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi, kupitia bandali ya Dar es Salaam; Kituo kinachojengwa kurasini, sambamba na hilo ujenzi wa mnada mpya wa kuuza chai ndani ya kituo hicho cha Kurasini.
Eneo lingine ni kugharamia uanzishwaaji wa vitalu vipya vitakavyozalisha miche mipya ya chai milioni moja na nusu (1,500,000).
Eneo lingine ni kutoa mafunzo ya elimu ya biashara kwa Wazalishaji na Wafanyabiashara wa mazao yenye thamani kubwa kama mbogamboga, matunda na viungo pamoja na kuandaa mifumo itayosaidia kujenga masoko ya mazao hayo (Matunda, mbomboga na viungo).
Naibu Waziri Hussein Bashe aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizonufaika na msaada wa fedha hizo katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Bashe amesema msaada wa fedha hizo utatolewa katika kipindi cha miaka minne huku kiasi cha Euro milioni 48 kitaenda kwenye kugharamia ujenzi wa miundombinu ya barabara za vijijini yalipo mashamba ya chai katika mikoa inayolima chai nchini na kuongeza kuwa ujenzi wa barabara hizo utaokoa kilo za chai zaidi ya milioni nne (4,000,000) ambazo zimekuwa zikipotea kila mwaka. Sawa na bilioni 3.8 fedha ambazo zingepatikana baada ya kuuza chai nje ya nchi kila mwa
“Euro milioni 48 zikazokwenda kwenye ujenzi wa miundombinu ni muhimu kwa kuwa tumekuwa tukipoteza zaidi ya kilo milioni 4 za majani ya chai mabichi ambayo yamekuwa yakitupwa kila mwaka kutokna na miundombinu mibovu”. Amekaririwa Naibu Waziri Bashe.
Post A Comment: