Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akifungua Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amewataka madiwani kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Mboje ameyasema hayo leo Jumanne Februari 16,2021 kwenye Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021 uliofanyika katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Iselamagazi – Nindo ukiwa na lengo la kujadili miradi inayotekelezwa katika halmashauri hiyo.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema ili kumaliza changamoto ya vyumba vya madarasa na madawati, Madiwani wanayo nafasi kubwa ya kuwahamasisha wananchi kuchangia badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
“Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga tunataka kutoka kwenye hali ya wanafunzi kukaa chini. Hamasisheni wananchi kuchangia madawati. Lakini pia hakikisheni viongozi wa vitongoji wanashirikishwa katika mambo ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa kuhusu fedha za zinazotoka serikali kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo”,alisema Mboje.
Katika hatua nyingine aliwataka TANESCO, RUWASA, TARURA na Idara ardhi wawe na mawasiliano kwa sababu wote wanafanya kazi ya jamii katika kuweka vizuri miundo mbinu.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Christina Mnzava alisema ili kupiga hatua za kimaendeleo ni lazima madiwani na wabunge na watendaji wa serikali washirikiane.
Aidh aliwasihi madiwani wa halmashauri hiyo kujiunga na Mifuko wa Bima ya Afya na kuomba Mfuko wa bima ya afya kutoa mkopo wa vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya.
Katika Mkutano huo, madiwani wamepaza sauti kuhusu changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambapo baadhi ya barabara zimekatika na madaraja hayapitiki hivyo kuiomba Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuzifanyia kazi barabara zinazolalamikiwa.
Walizitaja baadhi ya barabara zinazotakiwa kufanyiwa kazi kuwa ni pamoja na Barabara ya kutoka Didia – Solwa, Imenya – Usule- Mwamala na madaraja ya Nduguti – Igembya na Mimbi – Ikota na maeneo mengine ikiwemo miundombinu ya barabara katika Mji wa Didia.
Suala jingine lililoibuka katika mkutano huo ni changamoto ya miradi ya maji kutokamilika kwa wakati na miradi kutoendana na mikataba.
Diwani wa kata ya Mwakitolyo, Masalu Nyese aliiomba RUWASA kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kata hiyo ambao umekuwa ukisuasua na hivi sasa umesimama kwa takribani wiki mbili kutokana na upungufu wa mabomba hali inayosababisha wananchi kuendelea kukabiliwa na changamoto ya maji.
Masalu ametumia fursa hiyo kumuomba Mwekezaji katika mgodi wa Mahiga kuajiri vijana kwa mkataba maalumu badala ya utaratibu uliopo sasa ambao haueleweki.
Akizungumza katika mkutano huo, Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi alisema watatembelea barabara zenye changamoto na kuchukua hatua huku Kaimu Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi akisema wataendelea kutekeleza miradi ya maji kama inavyotakiwa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambaye ni Diwani wa kata ya Mwalukwa Mhe. Ngassa Mboje akifungua Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021 uliofanyika katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Iselamagazi – Nindo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambaye ni Diwani wa Kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengelema. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambaye ni Diwani wa kata ya Mwalukwa Mhe. Ngassa Mboje akifungua Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambaye ni Diwani wa Kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengelema akizungumza kwenye Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021 uliofanyika katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Iselamagazi – Nindo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza kwenye Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Christina Mnzava akizungumza kwenye Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akiongoza Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa Robo ya Pili ya mwaka 2020/2021
Afisa Uanachama NHIF mkoa wa Shinyanga, Errison Halinga akiwaelezea Madiwani kuhusu umuhimu wa bima ya afya
Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambi akielezea kuhusu miradi ya barabara
Kaimu Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi akielezea kuhusu miradi ya maji
Madiwani wakiwa ukumbini
Madiwani wakiwa kwenye kikao
Diwani wa kata ya Mwakitolyo, Masalu Nyese akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa kata ya Solwa, Awadhi Mbaraka akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.
Post A Comment: