HERI SHAABAN (MOROGORO)
MGANGA MKUU wa halmshauri ya Mvomero Mkoani Morogoro Dkt.Mwanamisi Hassan ametoa agizo kwa Maafisa Maendeleo wa Kata na Maafisa Ustawi wa Jamii wote wa halmashauri hiyo kutoa elimu dhidi ya Unyanyapaa kwa watu wenye Ulemavu ngazi ya Jamii na kusaidia uundwaji wakamati za watu wenyeulemavu katika ngazi zote.
Dkt. Mwanamisi Hassan aliyasema hayo Tarafa ya Turiani Mvomero Mkoani Morogoro jana, alipokuwa mgeni rasmi katika mafunzo ya kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu kutoka vijijini mbalimbali vya tarafa ya Mtibwa, mafunzo yalioandaliwa na Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya Mvomero Elizabeth Urio kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya na wadau mbalimbali wakiwemo Sightsavers kupitia Mradi wa afya ya macho jumuishi (Boresha Macho)unaofadhiliwa na UKAID na kutekelezwa na uongozi wa mkoa kupitia halmashauri za wilaya.
"Natoa agizo kwa Maafisa Maendeleo wote na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha kamati za watu wenyeulemavu kuanzia ngazi ya kijiji zimeundwa nakujengewa uwezo pia kushuka katika jamii kutoa elimu na kuwafanya uhakiki kuwatambua Watu Wenye Ulemavu wote hii itafanya Watu Wenye Ulemavu kutambulika na kujiamini pia kujitokeza katika masuala mbali mbali ya Kijamii na Kiuchumi " alisema DKt Mwanamisi
Dkt Mwanamisi alisema kwamujibu watakwimu kata ya mtibwa inavijiji 130 na kati ya hivyo vijiji 80 ndivyo vyenye kamati za watu wenyeulemavu.
"Natoa agizo kamati hizo ziundwe" Vikundi viundwe na vielimishwe majukumu yake, tunawadau wenye nia nzuri yakushirikiana na serikali kutatua changamoto zawatu wenyeulemavu bila kuwa na utaratibu wakuwafikia watu wenyeulemavu tutashindwa, miongozo ipo na sheria ya watu wenyeulemavu ya 2010 inaeleza vizuri, hivyo tuzitumie na watu wenyeulemavu wapate haki zao.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro Jesca Kagunila alitoa elimu ya uundwaji wa kamati za watu wenyeulemavu na umuhimu wake kama nyenzo yakudai haki na huduma kwawatuwenye ulemavu.
Aidha, ameridhishwa na kasi ya halmashauri yakutenga bajeti
kwajili ya kuimarisha huduma kwa watu wenyeulemavu.
Afisa Ustawi Jesca aliwataka wajiunge katika vikundi mbali mbali wapate fursa ya kupata mikopo hasa ile 2% inayotengwa na halmashauri.
Katika kongamano hilo la mafunzo wezeshi kwa watu wenyeulemavu lililohudhuliwa na watu wenye ulemavu takriban 204, wamepata mafunzo yanamna yakujiunga na bima ya afya iliyoboreshwa iCHF. Wamesisitizwa kujiunga katika mfuko huo iliwaweze kupata huduma za afya za uhakika.
Wadau mbalimbali wamehimizwa kufanyakazi kwaushirikiano ilikuwafikia watu wengi wenyeulemavu, shirika lisilo la kiserikali litwaalo New Hope Community development limeahidi kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu iliwaweze kujikwamua kiuchumi.
Shirika la Akoka kupitia USAID wanawajengea uwezo watoa huduma wa afya waangazi ya jamii na kusaidia kuwapatia iCHF watu wenyelemavu watokao kaya maskini.
Mratibu wa Mradi toka Shirika la Sightsavers wa Boresha Macho Magdalena Focus ametoa elimu juu ya huduma za macho jumuishi zinazotelewa na shirika hilo kwakushirikiana na halmashauri
Magdalena alisema Wadau hao wakifanyakazi kwa ushirikiano watu wenyeulemavu watapata huduma thabiti zaidi ya moja,na halmashauri itahakikisha inaratibu vyema utendaji huo.
Mratibu Magdalena alisema shirika linashirikiana na serikali kuboresha mifumo ikiwemo wa upatikanaji wa takwimu na utatuaji wa changamoto zawatu wenyeulemavu kupitia mabaraza yao, hivyo basi hawana budi kushirikiana kuunda mabaraza hayo na kuitikia fulsa zilizopo, ikiwemo hii ya matibabu ya macho.
Post A Comment: