Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ameanza kuboresha miundombinu ya viwanja mbali mbali vya michezo katika Jiji la Dodoma kwa lengo kukuza michezo na kuibua vipaji mbalimbali.

Mh Mavunde amebainisha hayo jana wakati akizindua viwanja viwili vya michezo alivyotengeneza miundombinu yake vilivyopo Mtaa wa Chizomoche,Kata ya Mbabala ambavyo sasa vinatoa fursa kwa wananchi kuweza kushiriki katika michezo katika mazingira rafiki.


“Azma yangu ni kuboresha michezo katika Jiji la Dodoma kwa kuboresha miundombinu ya viwanja na hivyo kuweka mazingira mazuri ya shughuli za michezo.


Kwa hivi sasa nimeshaweka magoli ya chuma na kuboresha miundombinu ya Viwanja vya michezo 16 vya maeneo mbalimbali,lengo langu ni kuzifikia kata zote 41 za Jiji la Dodoma na kuongeza hamasa ya michezo kote”Alisema Mavunde


Aidha wananchi wa Mtaa wa Chizomoche wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Mbabala **Mh. Paskazia Mayalla **wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa  kuwawekea vijana mazingira rafiki ya kushiriki katika michezo na hivyo kuwaondoa katika ushiriki wa vitendo viovu vyenye kuathiri Afya na tabia za Vijana.

Share To:

Post A Comment: