Ferdinand Shayo ,Manyara
Mshindano ya Sed Miss Valentines 2021 yamefanyika katika viwanja vya Champions Lounge vilivyopo mji wa Babati na Kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Babati pamoja na Viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Babati.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wamedhamini mashindano hayo ili kuendelea kutangaza kinywaji cha Sed ambacho kinafanya vizuri katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mulokozi amesema kuwa Wataendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ambayo yanalenga kutoa fursa kwa vijana wa Mkoa wa Manyara .
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amepongeza kampuni ya Mati Super Brands kwa kuwa karibu na jamii na kujitoa katika shughuli za kijamii pamoja na michezo.
Kwa upande wake Mrembo aliyenyakua taji la Sed Miss Valentines 2021,Upendo Blasi ameeleza furaha yake baada ya kushinda na kuahidi kuwa balozi mzuri wa Sed.
Post A Comment: