Na Raheem Secha,Songwe
Kampuni ya Majinja Logistics Company inayo chini ya Mkurugenzi wake Alnanuswe Kabungo imetekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda kwa vitendo Mkoani Songwe baada ya kujenga viwanda vitatu kwa mpigo.
Kata ya Igamba iliopo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ndipo Kampuni hii ilipojenga Viwanda vyake vya kukoboa Kahawa,kukamua alzeti na kiwanda cha Unga wa Mahindi.Meneja wa uzalishaji Viwanda vya Majinja Mkoani Venansi Ngoya ameleza kuwa wao kama Majinja wamewekeza Viwanda akiamini watawasaidia wakulima waliopo Mkoani Songwe na Mikoa ya jirani pia amesema wanatarajia kutoa ajira kwa Vijana na kina mama katika Viwanda vyao.
"Hapa tuna viwanda vitatu vinajengwa kiwanda cha kukamua alzeti,kiwanda cha Unga na kiwanda cha kahawa hivi vyote mwaka huu 2021 vitaanza kufanya kazi na tutatoa ajira nyingi ikiwa sambamba na kuwanufaisha wakulima kwa kununua mazao yao" amesema Venansi
Aidha Mkugenzi wa Majinja Logistics Ltd Alinanuswe Kabungo amesema wao kama kampuni wanamuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli sera ya Tanzania ya Viwanda na wameamua kuwekeza katika Mkoa wa Songwe na pia wapo Mkoa wa Mbeya kwa kiwanda cha Maji ya Tukuyu kilichopo Tukuyu na wameweza kutoa ajira nyingi kama kampuni hivyo ameshukuru Viongozi wanaotembelea shughuli zao na kuwashauri akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Generali mstaafu Nikodemas Mwangela.
Kampuni ya Majinja pia ni wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoa mbali mbali pia wanamiliki maloli ya kusafirisha mizigo nchini na nje ya nchi.
Post A Comment: