Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt Christowaja Ntandu(katikati) akifungua rasmi Kongamano la kumbukizi la Vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni wa kabila la Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Kulia kwake ni Bw Musa Nkolabigawa (mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma) na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na wadau katika Kongamano la kumbukizi ya Vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni wa kabila la Mkoa wa Ruvuma mjini Songea
Chifu Emmanuel Zulu wa kabila la Wangoni akifafanua jambo kwenye Kongamano la kumbukizi ya Vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni wa kabila la Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.
Wadau mbali mbali wakimsikiliza Chifu Emmanuel Zulu wa kabila la Wangoni kwenye Kongamano la kumbukizi ya Vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni wa kabila la Mkoa wa Ruvuma mjini Songea
…………………………………………………………………………………………………..
Na Sixmund Begashe
Wadau wa mbali mbali wa Utalii wa Utamaduni nchini wametakiwa kutumia makongamano kujadili namna gani tunaenzi na kuishi uzalendo na utamaduni wa umoja na kujitoa ambao ulipiganiwa na wazee wetu pia kuhakikisha uboreshaji na kuthamini urithi huo wa kihistoria na kiutamaduni wetu.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Aloyce Nzuki katika hutuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt Christowaja Ntandu kwa niaba yake katika ufunguzi wa Kongamano la kumbukizi la Vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni wa kabila la Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.
Dkt Nzuki ameeleza kuwa nia ya Wizara kwa sasa ni kutumia Matamasha na maeneo ya kihistoria kama mazao ya utalii ili wananchi wapate fusa si tu kwaajili ya kuhifadhi bali kutumika kama fursa ya kuongeza kipato cha kila mmoja na kukuza uchumi wa nchi.
“Nimatumaini yangu kuwa mawasilisho na majadiliano yatajikita katika kuibua mbinu za namna ya kuboresha historian a utalii huu wa Utamaduni si tu kwa Mkoa wa Ruvuma bali ni wa mikoa yote ya Kusini nan chi yote kwa ujumla” Ilieleza hutuma hiyo.
Akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa nchini Dkt Noeli Lwoga ameeza kuwa kongamano hilo ni muhimu katika kujadili masuala mbali mbali yanayohusu uhifadhi na uendelezaji wa Kumbukumbu za Vita ya Maji Maji, pamoja na masuala mengine yanayohusu urithi wa utamaduni wa Mtanzania.
“Aidha, Kongamano hili la Wadau ni la 12. Kuna haja ya kutathmini ni namna gani majumuisho ya Makongamano haya yanaboresha usimamizi wa urithi, na hasa namna yatachukuliwa na kufanyiwa kazi na Wadau na Wasimamizi wa Urithi. Ni muhimu pengine, hapo baadaye, kabla ya kila Kongamano tukafanya tathmini kidogo – pengine hili litawezekana katika Makongamano yajayo, na hasa kama tukiweka mkakati huo sasa” Alisema Dkt Lwoga.
Nae Chifu Emmanuel Zulu wa kabila la Wangoni ameitaka jamii ijifunze kupitia historia ya Mashujaa wa Vita vya Maji Maji na kuwaenzi kwa vitendo kwa kutanguliza uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuliletea taifa letu maendeleo na kila mmoja anufaike na matunda ya uzalendo huo.
“Kongamano hili ni muhimu sana tena sana maana linatup a nafasi ya kusikia michango mbali mbali kutoka kwa wadau wa urithi wa Utamaduni hasa huu wa makabila ya hapa Mkoa wa Ruvuma, hivyo nitoe wito kwa serikali kuendelea kufanya makongamano haya mara kwa mara ili kuboresha uhifadhi na uendelezaji wa urithi wa Utamaduni wetu” Aliongeza Chifu Zulu
Mada zilizo wasilishwa katika Kongamano hilo ni pamoja na “Dhima ya Methali za Wazee wetu zinavyosawiri maisha ya sasa” iliyowasilishwa na wazee wa Mila na desturi Mkoa wa Ruvuma, “Kanuni ya Majengenelu ya Mashujaa wa Maji Maji- Msingi wa Kujenga Taifa na Uzalendo kwa Tanzania” iliyowasilishwa na Dkt Xaver K. Komba na “Wazee wetu, historia yetu na fahari ya Taifa la Tanzania iliyowasilishwa na Dkt Oswald Masebo
Post A Comment: