Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi
Edmund Seif kulia akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao |
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif kushoto akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao |
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi Edmund Seif kushoto akisistiza jambo kwa Bodi ya Wakurugeni ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wakati wa ziara yao |
Bwawa la Nyumba ya Mungu kama linavyoonekana |
JAMII zinazoishi kando kando ya bwawa la Nyumba ya Mungu
wameshauri kuacha shughuli zitakazochangia kuharibu bwawa hilo bali
walinde na kutunza chanzo hicho ili kujihakikishia uzalishaji wa
uhakika wa nishati ya umeme hapa nchini.
Ushauri
huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Wakurungenzi ya Shirika
la Umeme nchini TANESCO Balozi James Nzagi wakati wa ziara yake ya
kukagua kituo cha kuzalisha umeme cha bwawa la nyumba ya Mungu kilichopo
mkoani Kilimanjaro.
Alisema
kuwa maji ndio nishati inayotumika katika kuendeshea mashine za
kuzalisha umeme hivyo ipo haja ya jamii kuendelea kuelimishwa kulinda na
kutunza vyanzo vya maji ili kujihakikishia uzalishaji wa uhakika wa
umeme lakini na kwa ajili ya maendeleo yao.
"Jamii
inatakiwa kukwepa kufanya shughuli ambazo zinahataridha uhai wa maji
ya bwawa la mto wa Nyumba ya Mungu kwani maji hayo sio tuu yanatumiwa
na TANESCO bali hata wananchi wanategemea raslimali hiyo kwa matumizi
yao " alisitiza Makamu Mwenyekiti huyo.
Hata
hivyo aliwataka watumishi wa shirika hilo kuendelea kufanyakazi kwa
uwadilifi ikiwemo kujiepusha na vitendo ambavyo vitasababisha kushusha
hadhi yao na shirika kwa ujumla.
Vile
vile alisema kuwa licha ya kuwepo kwa mitambo mikongwe ya kuzalishia
umeme katiks baadhi ys vituo lakini ameweza kuridhishwa na namna
inavyofanyakazi kwa ufanisi kama mitambo ya kisasa.
"Hiki
nikichojionea ndio ile kauli ya Wahenga kwamba kitunze kidumu kwani
uimara wa mitambo hii inatokana na marekebisho yanayofanywa mara kwa
mara hii yote ni katika kuwahakikishia huduma bora watanzania" alisema
Balozi Nzagi.
Kwa upande
wake Meneja Mwandamizi Uzalishaji TANESCO makao makuu Steven Manda
alisema kuwa shirika hilo lipo kwenye maboresho ya mitambo yako kutoka
analogi kwenda kwenye digitali ili kuboresha utendaji wao wa kazi wa
kutoa hudums bora.
"Maboresho
hayo sasa yataweza kumaliza changamoto ya kukatika kwa umeme kwani kama
kuna hitilafu mitambo itakuwa inataarifa mapema na hivyo hatua za
marekebisho zinachukuliwa kwa haraka" alisema Manda.
Nae
Kaimu Mkuu wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu Mhandisi
Edmund Seif alisema kuwa kituo hicho kinazalisha umeme megawati 8 kwa
kutumia mashine mbili.
Hata
hivyo alisema kutokana na uwepo wa maji ya kutosha katika bwawa hilo
kwa kipindi cha miaka mitatu mfululuzi hawajawahi kuzalisha chini ya
kiwango.
Post A Comment: