Na Raheem Secha,Ileje
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude ameamuru Afisa Habari wa Ileje Daniel Mwambene awekwe ndani kwa kosa la kutowaalika Waandishi wa Habari katika Vikao muhimu vya serikali pia amempa maagizo Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi kubadili mfumo wa kuwaita Waandishi wa Habari
Akiongea na Mwandishi wetu Mkude amesema ameshangazwa na kitendo cha Waandishi wa Habari kutokuwepo katika Vikao muhimu kama kilichofanyika leo cha DCC
"Afisa Habari ni mratibu wa Waandishi wa Habari sio mwana habari leo wananchi wanakosa habari muhimu kama hizi sababu ya uzembe wa mtu mmoja serikali inafanya mambo kwa uwazi yeye anakuja kutoa taarifa za vikao baada ya wiki nimeamua kumuweka ndani ili iwe fundisho hatutaki mzaha" amesema Mkuu wa Wilaya
Post A Comment: