Nteghenjwa Hosseah, Songwe
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dr. Ntuli Kapologwe amechukizwa na kusua sua kwa ujenzi wa kituo cha Afya Kapele kilichopo katika Halmashauri ya Momba Mkoani Songwe.
Dr. Ntuli alionyesha hali hiyo wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi Mkoani Songwe na kutembelea kituo cha Afya Kapele kuangalia hatua za ujenzi zilizofikiwa.
“Kituo hiki kililetewa fedha mwaka 2018 shilingi Mil 400 na katika maeneo mengine ambayo wamepokea fedha hizo wameshakamilisha ujenzi na vituo vimeanza kutoa huduma sasa hapa kuna tatizo gani miaka mitatu kituo hakijakamilisha hii ni hujuma kwa Serikali”
“Hapa tungependa kusikia kutoka kwa watu waliohusika katika ujenzi wa Kituo hili kama Mkurugenzi, Mwekahazina, Mhandisi, Mganga Mkuu pamoja na Manunuzi ili tufahamu kwa kina kitu walitumiaje fedha zile mpaka zisitoshe kukamilisha ujenzi wa kituo hiki” alisema Dr. Ntuli.
Tumejenga zaidi ya Vituo 472 vyote kwa gharama mil 400 kwa kila kimoja na vyote vimekamilika hapa kuna tatizo gani mpaka mnaomba fedha zaidi ya shilingi Mil 300 ili mkamilishe ina maana mtakua mmejenga kwa Mil 800 na zaidi hii sio gharama ya kituo cha Afya ni ya Hospitali ya Wilaya aliongeza Dr Ntuli.
Akisoma taarifa ya ujenzi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Momba alisema Halmashauri ilipoeka shilingi mil 400 na ujenzi ulianza mwaka 2018 na majengo yanayojengwa jengo la wagonjwa wa nje, maabara, chumba cha upasuaji, afya ya uzazi pamoja na wodi ya kinamama.
Kaimu Mkurugenzi huyo alidai kuwa fedha hizo ziliisha kabla majengo hayo hayajakamilika hivyo Halmashauri iliongeza shilingi Mil 86 huku nguvu za wananchi zikiwa na thamani ya mil 18.3.
Aliongeza kuwa wamewasilisha maombi Ofisi ya Rais -Tamisemi ili waweze kupatiwa shilingi mil 312 kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo.
Timu ya usimamizi shirikishi Mkoani Songwe ilifanya kikao na Timu ya Mkoa ya usimamizi wa huduma za Afya na kutembelea Kituo cha Afya Kapele pamoja na Ndalamo.
Post A Comment: