OR-TAMISEMI, MTWARA
Mkurugenzi wa Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Ntuli Kapologwe amezitaka timu za uendeshaji na usimamizi wa huduma za Afya za Halmasahuri kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma ili vituo hivyo viweze kujiendesha katika siku za usoni.
Dkt. Ntuli aliltoa rai hiyo katika kikao chake na timu za endeshaji na usimamizi wa huduma za Afya (CHMT) za Mkoa wa Mtwara wakati wa ziara ya Usimamizi shirikishi Mkoani humo.
Dtk.Ntuli alizitaka timu hizo kubadilika na kuacha kutegemea fedha kutoka Serikali kuu ila wahakikishe kuwa kila kituo kinakusanya fedha za kutosha kuweza kujiendesha hata kama fedha zisipoletwa.
“Ukusanywaji wa fedha bado unasuasua, hamko makini katika ukusanyaji wa mapato, haiwezekani kituo cha afya kinakusanya elfu tatu kwa siku ina maana hamtoi huduma au fedha zinakusanywa lakini zinapita mikononi mwa watu,nahitaji umakini katika ukusanywaji wa fedha” alisema Dr. Ntuli.
Fedha zinazokusanywa ndizo zinazotumika katika uendeshaji wa huduma za afya katika vituo vya afya, kushindwa kukusanya fedha hizo ni uzembe wa hali ya juu na kukosekana kwa umakini katika utendaji wenu, imarisheni ukusanyaji wa mapato ili twende sawa” Alisema
Mkikusanya mapato ipasavyo Kituo hakitakosa dawa hata siku moja maana mtakua na uwezo wa kununua dawa za kutosha, stahiki za watumishi zitalipwa kwa wakati na fedha za uniform pia zitakuwepo, hamtakuwa na changamoto ndogondogo; Haya yatatokea endapo tu mtakua makini katika ukusanyaji wa mapato na kutumia mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji.
Katika kufanikisha azma hii ya kuongeza mapata lazima mfungue maduka ya dawa katika Vituo vya Kutolea huduma hii ni miongoni mwa vyanzo vya uhakika vya mapato katika vituo vyenu.
Nataka mpunguze utegemezi wa fedha za mfuko wa pamoja ina maana siku zisipoletwa mnafunga vituo simamieni mapato vizuri muweze kujitegemea alimalizia Dr.Ntuli.
Post A Comment: