Jane Edward,Msumba News,Arusha


Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ameiomba Serikali kuhakikisha wanazisaidia Taasisi za mboga mboga  nchini kwani zimekuwa zikifanya utafiti unaoaminika na kuwafikia wanajamii.


Ametoa wito huo mara baada ya kuzindua jengo la kituo cha  kimataifa cha utafiti wa mazao ya mboga za asili ya kiafrika (World Vegitable Center )lililopo Tengeru jijini Arusha.


Pinda amesema kuwa, pamoja na kituo hiki kuwa na sifa nyingi zinatakiwa zipewe kipaumbele na serikali ili kuhakikisha zinafikia malengo mazuri waliojiwekea.


Pinda aliongeza kuwa,kwa ilani ya chama ya mwaka 2020-2025 kuna maeneo mengi yanayozungumzia juu ya uimarishaji na uendeleshaji wa taasisi za tafiti hizo kwani zina mchango mkubwa katika nchi.


Aidha amewataka vijana hao kuzitumia taasisi hizo  kwa ajili ya kupata mbegu bora za asili na kuboresha shughuli mbalimbali za kilimo na hatimaye kuweza kupata kipato chao na Taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho, Dokta Gabriel Rugalema amesema kuwa, kupitia kituo hicho  kimekuwa kikitoa  mchango mkubwa kwa wakulima, ,watafiti , pamoja na wananchi kwa ujumla.


"jukumu letu kama kituo ni kuhakikisha tunawafundisha wanasayansi, wakulima na vijana kuhusu kilimo cha  bora cha mboga mboga"alisema Rugalema.


Rugalema ametoa wito kwa wadau mbalimbali pamoja na serikali kuwa kama wanahitaji kuondokana na magonjwa mbalimbali ni lazima kuzingatia kilimo cha mboga mboga ili kuimarisha afya zetu kwa ujumla.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: