NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi amesema kuwa jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono maonesho na matamsha yanayohusisha wasanii na kazi  za utamaduni kwani matokeo ya muziki uwafikia mamilioni ya watu ulimwenguni.


 


Kenan aliyasema hayo wakati akifungua Tamasha la maarifa, sanaa na kujenga mtandao  (KANFESTIVAL) kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, lililoanza leo katika chuo cha maendeleo na ushirikiano wa kimataifa(MS-TCDC) ambapo alisema kuwa wanapojadili, kulumbana, kuimba na kutazama maonesho ya Kan kwa siku hizo tatu wajikite katika kuelekeza juhudi za maendeleo.


"Tunahakikisha tunaendelea kuhisaidia sekta hii muhimu ya uchumi na kukaribisha ushirikiano ambaoutaimarisha sekata hii kwa maendeleo ya taifa zetu,"Alisema Kenan.



Aidha alieleza kuwa uhuru wa wasanii kuwa haki kujieleza na ubunifu haipaswi kuzuiliwa japo ubunifu na uhuru wa kujieleza sio kitu pekee kinachowatafsiri wao kama wasanii ila utambuliwa kwa kazi zao  lakini uhuru wa kujieleza na kuwa wabunifu ni muhimu. 



Mkurugenzi wa Tamasha hilo kwa mwaka huu wa 2021  Bi Khalila Mbowe alisema kuwa tamasha la Kan linawasaidia wananchi kujisikia kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya nchi zao  kwa kujiona wao ni fursa  ya ndio majawabu ya kusukuma gurudumu la maendeo ya Afrika.


Alieleza kuwa tamasha hilo litahudhuriwa na waasanii mbalimbali wa muziki kutoka nchi za Afrika mashariki akiwemo G nako, Nikki wa pili Nazizi Grece Matata, Tarajazz Richie, Worriors from the East na Dj Skadi ambapo limeanza January 28 na kuhitimishwa January 30 huku asilimia 85 ya tamasha hilo likifanyika mtandaoni kutokana na changamoto ya Corona inayoendelea kuikabili dunia hivi sasa.


Bi Khalila Mbowe mkurugezi  kwa mwaka huu kuna utofauti mkubwa ambao ni tamasha kufanyika kwa asilimia kubwa mtandaoni, mijadala,  kuboresha afya kwa kuwa na mbio maarufu Kan run,  pamoja na Kan harcks.


Alisema lengo lao ni kujimuisha bara zima la Afrika bado ndio maana wote ambao ni marafiki wa maendeleo ya afrika wanashiriki Kan Festival kupitia mijadala itayoendeshwa katika mitandao ya kijamii na kuona ni jinsi  gani wanaweza kukuza maendeleo ya bara la Afrika hasa kwa kuangalia agenda ya 2063 ya umoja wa mataifa.


“Kususudi la Kan Festival na huu ni mwaka wa tatu na inaendelea kukua na kuonekana ulimwenguni na kwa mwaka huu kutakuwa na mijadala tofauti tofauti hapa na kwenya Mitandao pia na lengo ni moja kuhakikisha tunapotoka hapa tunasemaje au tunatokaje Kama washiriki wa mjadala,” Alisema Sara Teri.


Alifafanua kuwa mara nyingi watu wa kawaida wanakosa fursa ya kujadili maendeleo ya bara lao na badala yake Kuna kuwa na watu wanaojadili bila sauti za watu wa kawaida kusikika zikionyesa jinsi wanavyoshiriki au kuhusika hivyo lengo ni wewe na yeye mnasemaje juu ya maendeleo ya bara.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: