Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akimkabidhi vifaa tiba Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia) wakati wa kikao cha kutathmini maendeleo ya Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 

Shirika la World Vision limetoa msaada wa vifaa tiba na vifaa vya kuanzishia huduma ya Tiba Mtandao vyenye thamani ya Shilingi Milioni 148.8 ili kukinga magonjwa ya kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga. 

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Jumanne Disemba 8,2020 na Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ndugu Albert Msovela wakati wa kikao cha kutathmini maendeleo ya Mradi wa ENRICH kilichofanyika katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga.  

Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa Ufadhili wa Serikali ya Canada Dk. Frank Mtimbwa amesema vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi 148,816,000/= vitagawiwa katika halmashauri zote sita za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kahama Mji, Msalala, Ushetu,Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kishapu.  

Amevitaja vifaa hivyo kuwa ni Smart Tv ,Oxygen Cylinder,Nebulizer compreser, Nebulizer Mashine, Suction mashine leg operator, Suction mashine heavy duty, Pulse Oximeter, Oxygen nasal catheter, Mashine za kupimia msukumo wa damu mwilini (BP Machine) na Infra –led thermometer.  

Vifaa vingine ni mifuko ya kuhifadhia taka hatarishi (Biohazards bags), Dawa maalumu za kutakasia (Disinfectants) zenye ujazo wa lit 5 kila moja, vikinga uso wakati wa kumuhudumia mgonjwa (Protective face shields na Eye Protective googles), P/50 surgical gloves, Examination gloves, Barakoa tiba (surgical masks), hand washing soap, Hand washing system 100Lts na Hand washing system 50Lts. 

Amesema vifaa hivyo kupitia mradi wa ENRICH unaolenga kuboresha lishe ya mama na mtoto unaotekelezwa katika halmashauri tatu za wilaya kati ya 6 za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Shinyanga na Kahama Mji. 

“Tunapofikia mwisho wa huu mradi tumeangalia changamoto zinazotukabili tumeona leo tukabidhi vifaa hivi kwa ajili ya kuokoa maisha katika halmashauri zote za wilaya mkoani Shinyanga”, amesema Dk. Mtimbwa. 

“Pia mradi umefanya tathimini kwa kushirikiana na Wizara ya OR TAMISEMI, Wizara ya Afya, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Halmashauri kwa ajili ya kuanzisha huduma ya Tiba Mtandao ili kupunguza changamoto zinazowakabili watoa huduma wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya ambavyo vina changamoto ya watumishi.

 Hivyo tunahitaji wawe wanapata ushauri wa Kibingwa kabla ya kumpeleka mgonjwa sehemu nyingine ili kupata matibabu zaidi. Kwa maana hiyo kuna baadhi ya vituo vya vitafungwa mfumo wa Tiba Mtandao hasa zile za ngazi ya chini kabisa ya rufaa ambavyo tutavikabidhi Runinga”,ameongeza. 

Akipokea vifaa hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amelishukuru Shirika la World Vision kwa msaada huo wa vifaa tiba vya kisasa ili kuwezesha vituo vya afya kutoa huduma za kisasa zaidi. 

“Serikali ya mkoa wa Shinyanga tunawashukuru World Vision kwa msaada huu mkubwa kwa sababu sasa vituo vyetu vya afya japo siyo vyote tunaenda kupunguza changamoto zilizopo. Nina imani watalaamu wetu wa afya watatumia vifaa hivi kuboresha huduma za afya na kutumia vifaa hivi kwa malengo yaliyokusudiwa na tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi katika kuboresha huduma za afya”,ameongeza Msovela. 

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile amesema vifaa hivyo vitasaidia katika masuala ya lishe na kuokoa akina mama wajawazito hasa wanapokuwa katika eneo la Upasuaji na mfumo wa mawasiliano katika kuhakikisha huduma ya upasuaji kwa njia ya mtandao au ushauri kwa njia ya mtandao vitafungwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
 Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akimkabidhi vifaa tiba Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia) wakati wa kikao cha kutathmini maendeleo ya Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kilichofanyika leo Jumanne Disemba 8,2020 katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog  
 Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akilishukuru Shirika la World Vision kutoa msaada wa vifaa tiba na Tiba Mtandao kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.
Kulia ni Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akionesha sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision ili kukinga magonjwa ya kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga. 
Kulia ni Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akionesha sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision ili kukinga magonjwa ya kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga. Pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (wa tano kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yudas Ndungile (wa kwanza kushot) na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akionesha sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision ili kukinga magonjwa ya kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga. Pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (wa tano kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yudas Ndungile (wa kwanza kushot) na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga.

Kulia ni Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank Mtimbwa akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba ili kukinga magonjwa ya kuambukiza na kusaidia matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga. 
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba vilivyotolewa na Shirika la World Vision kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.
Muonekano wa moja ya Tv/Runinga zitakazofungwa mfumo wa Tiba Mtandao zilizotolewa na Shirika la World Vision kwa ajili ya vituo vya afya mkoani Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share To:

Post A Comment: