MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwijuma alimaarufu "Mwana FA" kushoto
akimueleza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ukubwa wa
tatizo la maji wilayani Muheza wakati wa ziara yake |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kulia akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake wilayani Muheza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi Mwinjuma Alimaarufu Mwana FA
WIZARA ya Maji imehaidi kupelekea fedha wilayani Muheza
Mkoani Tanga ili mradi wa kutoa maji eneo la Pongwe wilayani Tanga hadi
Kitisa wilayani Muheza ulioishia njiani uweze kusambaa kwa wananchi ili
kupunguza changamoto ya tatizo la maji wilayani humo.
Hayo
yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga
wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo ambapo alisema fedha
hizo ambazo makadirio yake ni Bilioni 4 watazipeleka kidogo kidogo mpaka
zitakapokamilika
Alisema
ni kweli fedha hizo ni nyingi lakini hawawezi kuzipata kwa mkupuo
watakuwa wakipeleka kwa awamu wanaweza kutumia na kuangalia wapi
wamebakiza na maelezo yake ni kwamba mradi mkubwa wa kutoa Maji Mto
Pangani utakapoanza uungane na mradi ambao unaendelea.
"Niwahakikishie
wananchi wa Muheza wizara ya maji haitakuwa kikwazo kuwapatia huduma ya
maji najua tumechelewa hivyo mwezi Desemba tutawaletea fedha mfanye
manunuzi ya mabomba na kabla ya mwezi huu haujaisha tuone mmeanza
kuchimba mitaro na kulaza mabomba naliongea hili kwa sababu Rais Dkt
John Magufuli alihakidi kwenye kampeni anataka wananchi wapate
maji”Alisema
Aidha
alieleza pia Rais Dkt John Magufuli alisema na serikali anayoiongoza
haitavumilia kuona wananchi wanakosa maji na aliwalenga wananchi
wanyonge hivyo raisi ametoa fedha kupitia mfuko wa maji na wanaangali
maeneo yeye shida ya maji na wanapeleka na kueleza mradi wa maji wa Mto
Pangani upo njiani.
“Lakini
niwahaidi kwamba wizara ya maji haitakuwa kikwazo kwenye suala la maji
wilaya muheza nimepitia ripoti kwa kweli hazipo vizuri kwenye wilaya ya
Muheza na Mkinga kuna changamoto kubwa ya maji nimetoa maelekezo bahati
nzuri wataalamu wa wizara ya maji wamekwisha kuingia wataanza
kushughulika na Mkinga”Alisema
Alisema
kwa bahati nzuri wilaya ya Muheza walikwisha kufanya kazi nzuri ya
kutoa maji Pongwe mpaka Kitisa na yamesogea kilomita sita kuna bomba
halijaakaa vizuri nalifahamu hilo ila kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani
lakini hatuwezi kusubiri mradi huo.
“Nafahamu
kuna mradi mkubwa wa Mto Pangani lakini hatuwezi kusubiri mradi huo
kama maji ya Tanga yanaweza kufika hapa na bahati nzuri Muheza
tumeikabidhi Tanga Uwasa na nimekwisha kuwaeleza leo kwamba lazima
huduma ya maji Muheza ifanane na Tanga mjini na Pangani kwa hiyo
watashughulikia”Alisema
Awali
akizungumza wakati wa ziara, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Hamisi
Mwinjuma almaarufu Mwana FA alisema maji ndio tatizo kubwa kwenye Jimbo
hilo na nililiahidi wakati wa kampeni na hata Rais alipotembelea mkoa wa
Tanga tukiwa Korogwe nililihubiri suala hili.
Mbunge
huyo alisema pamoja na kwamba serikali ya Rais Dkt John Magufuli
inafanya kazi nyingi nzuri lakini hili la maji linawaweka kwenye wakati
mgumu na watu hivyo wao wakamuomba tena mradi uliokuwa unatoa maji
Pongwe Kilapura ambao ulikuwa na Tanki la lita laki saba ulikuwa
umekwisha kuingiza maji NHC kwenye matanki.
Alisema
lakini tatizo likawa kwenye mfumo wa usambazaji na kukawa na maeneo
kwamba utafanayiwa kazi na hata Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi
Geofrey Hilly alipokuja na kutoa namba zake akawa mdomo wazi kwamba
kiasi cha fedha kinachoitajika ni bilioni 4 kwa hiyo mradi wa Bilioni
6.1 bado unahitaji bilioni 4 karibu asilimia 40 mradi haujakamilika.
“Ombi
langu kwao toeni fedha kwenye mfuko wa maji japokuwa wazo la awali
lilikuwa kusubiri mradi wa kutoa maji Mto Pangani utakaoanza mapema
mwakani ingawa utachukua muda mpaka kukamilika na kufika kwa
wananchi”Alisema Mbunge huyo.
Mbunge
Hamisi alisema wanawashukuru wizara hiyo kwa kusikiliza ombi lake
hivyo wanaomba huo mfumo wa utengenezwe kwa fedha kutoka mfuko wa maji
halafu mradi wa kutoa maji Pangani utakapofika watoe kiasi kilichokuwa
kimewekwa kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa usambazaji kiasi cha
bilioni 4.
“Kama
fedha zinarudi huko kwenye mradi mwengine zirudishwe huko lakini mfuko
wa maji uwasaidie kwa sababu wananchi wanateseka niishukuru serikali ya
awamu ya tano kuna sehemu maji yanatoka mara mbili kwa wiki na mara moja
kwa wiki masaa manne”Alisema
Hata
hivyo alisema pia kuna mahali maji yakitoka mara mbili kwa wiki
unapigiwa simu tatizo hilo ni deni kubwa kwake na serikali ya awamu ya
tano hivyo wanaomba lipatiwa ufumbuzi ili wananchi waweze kuondokana na
adha hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo |
Post A Comment: