Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wito umetolewa kwa wataalam wa ununuzi na ugavi kufuata sheria kanuni na taratibu zilizowekwa ili kuweza kukuza uchumi wa nchi yetu.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa idara ya ununuzi kutoka shirika la umeme Tanesco Nyalu Patson Mwamwaja wakati akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya kupokea hati ya shukrani ya kuthamini mkutano wa 11 ununuzi na ugavi uliofanyika katika ukumbi wa AICC uliopo mkoani Arusha
Alisema kuwa vyema wakaacha uzembe na wafanye kazi kwa weledi katika kusimamia mnyororo wa ununuzi na ugavi iliwasikwamishe utekelezaji wa miradi.
Alisema kuwa wameamua kuthamini kongamano hilo kwakuwa wao ni wadau wakubwa na shirika hilo kunatoa mchango mkubwa Sana katika fani hii ya ununuzi na ugavi
Alisema shirika la Tanesco ndilo linaloongoza kwa kuajiri wanunuzi wengi na wagavi ,ambao ni wafanisi na wanaoleta Maendeleo katika ufanisi endelevu wa nchi na wa fani hii kwa ujumla ,na waendelee kufanya kazi vyema kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.
Aliwataka waendelee kufuata sheria kanuni za maadili na kuendelea kutoa ushauri wa manunuzi kwa kufuata Sheria ya manunuzi ya umma .
Post A Comment: