Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Mhe.Deogratius Lukomanya(mgeni rasmi) akizungumza katika mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili (NVA Level 11) na la tatu (NVA Level 111)VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo VETA Chang'ombe Bw.Joseph Mwanda akizungumza mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili (NVA Level 11) na la tatu (NVA Level (111)VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanamitindo wakionesha mavazi ambayo yamebuniwa na wanafunzi wa chuo cha VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam katika mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili (NVA Level 11) na la tatu (NVA Level 111)VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam
Wanafunzi wa Chuo cha VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam wakiimba na wakicheza muziki (bendi) katika mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili (NVA Level 11) na la tatu (NVA Level 111)VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wahitimu wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA wametakiwa kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kujituma hasa kwa ujuzi walioupata Chuoni ili waweze kupata mafanikio.
Akizungumza katika mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili (NVA Level 11) na la tatu (NVA Level 111)VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Mhe.Deogratius Lukomanya amewataka waondokane na dhana ya kuletewa ajira bali wajitume kwa kujitengenezea ajira.
Alisema katika karne ya 21 upatikanaji wa ajira umekuwa ni changamoto kubwa ulimwenguni kote hivyo ni wajibu wenu kuwa na mawazo ya kujitengenezea ajira zenu wenyewe kwa ujuzi mliopata.
Aidha Mhe.Lukomanya amewataka wahitimu waendelee kuwa waminifu na moyo wa kufanya kazi kwa kujituma katika sehemu zao za kazi ili waweze kupata mafanikio.
Hata hivyo, amewaomba waajiri kuendelea kupokea vijana na kuwapatia nafasi za mafunzo kwa vitendo viwandani pamoja na nafasi za ajira kwa vijana pale zitakapopatikana.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo VETA Chang'ombe Bw.Joseph Mwanda amesema kuwa mwaka huu 2020 Chuo kimeweza kusajili jumla ya wanafunzi 1,361 wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu kwa kozi za muda mrefu na diploma ya ubunifu wa mitindo ya mavazi.
Amesema Chuo hicho kina wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu wa mfumo wa fahamu na watu wenye ulemavu wa viungo ambapo wengi wao wameonyesha uwezo mkubwa kwenye mafunzo yao.
" Kwa mwaka huu 2020 tuna wanafunzi wenye mahitaji maalumu 21 katika fani mbalimbali. Kati yao wanafunzi 10 ni wenye ulemavu wa mfumo wa akili na wanafunzi 11 ni wenye ulemavu wa viungo". Amesema Bw.Mwanda.
Hata hivyo Bw.Mwenda amesema changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na uhaba wa majengo na samani kwaajili ya wanafunzi wa kozi ndefu na fupi kwa karibu nusu ya mahitaji.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wote Bi.Avelina Mrema amewahimiza wahitimu kutokata tamaa katika maisha yao kwani ndio ukurasa mpya umefunguliwa.
Post A Comment: