Mawakala wakiwa katika zoezi la kuhesabu kura baada ya Uchaguzi huo. |
Bw. Danny Makange Msanifu Kilimo ambaye ni Katibu wa Baraza la michezo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumzia mipango mikakati ya baraza hilo jipya |
Na MwandishiWetu Dodoma
Viongozi wa Baraza la Michezo wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waliochaguliwa katika kinyanganyiro kikali cha kugombea nafasi za Mwenyekiti na Mwenyekiti Msaidizi wa Michezo, pamoja na nafasi ya Katibu mkuu na Katibu mkuu msaidizi, wameapa kukuza tasnia ya michezo katika Taasisi hiyo nakutumia fursa walioipata kutangaza shughuli za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupitia sekta ya Michezo.
Akizungumza baada ya uchaguzi huyo Mwenyekiti aliyeshinda Bw. Yassin Kazoba Ambaye ni mchumi, ametoa ahadi yakushirikisha watumishi wote wa Tume katika shughuli za michezo kwani Utendaji wa kazi unategemea afya za watumishi.
Katibu wa Baraza hilo jipya Bw. Danny Makange alisema anamkakati wakuainisha wachezaji katik a Ofisi za Tume nchi nzima ilikuweza kupata ushindani katika michezo ya mabonanza na mashindano mengine na mashirika naTaasisi za Serikali.
Pia kuunganisha wanamichezo na wadau ilikuwezesha taasisi na shughuli zake zifahamike.
Kwaupande wake Mkurugenziwa Utawala na Rasilimali watu Bi, MARY MWANGISA amewataka viongozi hao pamoja na kutekeleza wajibu katika shughuli za michezo, waongeze bidii ya kazi ili Taasisi hiyo iweze kufikia malengo ya kimkakati la kukuza eneo la Umwagiliaji zaidi la Hekta zaidi laki sita zinazomwagiliwa kwasasa,kufikia Hekta Milioni moja na laki mbili ifikapo mwaka 2025.
Awali Mwenyekiti wa uchaguzi huoBw, Godwin Mutahangarwa ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha sheria, amewataka viongozi hao kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kuushukuru uongozi wa Taasisi kwa kuunda chombo hicho ambacho ni muhimu sana na namna mojawapo yakuwashirikisha wafanyazaki na kujenga uhusiano mwema kati ya wafanyakazi na Taasisi naTaasisi.
Post A Comment: