NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Abdulrazak Batru amesema kuwa kuwa urejeshaji wa mikopo kwa waliochukua muda mrefu umeongezeka kutoka billion 30 za awali na kufikia billion 182.
Batru aliyasema hayo katika mahafali ya 10 ya chuo kikuu cha Tumaini Makumira ambapo alisema kuwa urejeshaji unazidi kuongezeka na mwaka huu wanatarajia kuwa na ongezeko kubwa zaidi hivyo wanapongeza wanaoendelea kurejesha ikiwa ni pamoja na kuwasihi wote wa waliokopa kurejesha ili fedha hizo ziweze kuaomesha watu wengine.
Alisema katika CHUO hicho wahitimu 400 ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na hayo ni matokeo ya kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya kuwalipia kutoka billion 420 hadi billion 480 kwa sasa ambapo amewahimiza wahjtimu hao kutumia maarifa yao ili kuweza kurejesha pesa walizokopeshwa.
“Wanaporejesha kwa wakati pesa hizo zina saidia kuwasomesha wanafunzi wengine hivyo nawasisitiza wanapomaliza masomo wajitahidi ni lazima wajitahidi kurejesha mapema,”Alisema
Aidha aliekeza kuwa serikali imeweka utaratibu ambao pesa ya wanafunzi wanaoingia vyuo vikuu inapatikana mapema ambapo hata sasa pesa ya wanafunzi wotw iltumwa kabla vyuo havijafunguliwa.
Kwa upande wake mkuu wa chuo kikuu hicho ambaye pia ni mkuu wa kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt Frederick Shoo aliwataka wanafunzi zaidi ya 1000 waliohitimu katika chuo hicho kwenda kutumia vizuri elimu waliyoipata kwa kuboresha na kuleta ufanisi katika katika fani zao.
Askofu Dkt Shoo alisema kuwa pamoja na wahitimu hao kwenda kuleta ufanisi katika fani zao pia tabia na mienendo yao ifanane na watu walioelimika.
Kutokana na wachungaji walio wengine kujitokeza kusoma elimu ya juu alieleza kuwa kanisa la sasa linahitaji wachungaji walioelimika ili waweze kukidhi mahitaji ya waaumini ambao kwasasa wengi wana elimu ya hali ya juu.
“Waumini hivi sasa asilimia kubwa wameelimika hivyo ni sahihi kabisa wachungaji kuongeza elimu ili kuweza kukidhi sifa za kuwaongoza waumini ambao wameelimika,” Alieleza Askofu Dkt Shoo.
Naye Profesa Esther Mwaikambo Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha Tumaini Makumira alieleza kuwa safari ya wahitimu hao haikuwa rahisi, lakini hivi sasa wameiva na wako tayari kutumikia jamii nakuwasihi wakaendeleze maadili mema waliyoyapata katika chuo hicho.
“Mnapoenda katika Jamii mtakutana na changamoto nyingi lakini mkawe wavumilivu na wenye hekima mkiendeleza maadili mema mliyoyapata katika chuo hiki, mkawe mabalozi wazuri katika kutangaza chuo chenu,” Alisema Profesa Mwaikambo.
Mmoja wa wahitimu wa chuo hicho wa shahada ya Theolojia Godson Moshi alisema kutokana na changamoto ya Corona iliyotokea mwaka huu, kumaliza kwao ni kwa neema ya Mungu hivyo jamii itegemee matunda mazuri kutoka chuo hicho katika kila fani.
Post A Comment: