Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali, akizungumza kuhusu matengenezo ya Mitambo na Magari yanayotumika katika Kilimo cha umwagiliaji na ujenzi wa miundombinu yake.Moja ya mtambo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Dodoma ukiwa Tayari kukodishwa kwa ajili ya Shuguguli za kilimo cha Umwagiliaji na Ujenzi wa Miundombinu yake.
moja ya gari lililopaki zaidi ya mwaka mmoja aina ya Nissan Diesel lenye namba za Usajili STJ 328, likifanyiwa matengenezo tayari kwa shughuli za umwagiliaji. |
Baadhi ya Magari yaliyopo tayari kukodishwa kwa ajili ya shughuli za kilimo cha Umwagiliaji na ujenzi.
NA MWANDISHI WETU,DODOMA
IMEELEZWA
kuwa katika robo ya pili ya mwaka wa Serikali,Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji inategemea na inaendelea kutekeleza majukumu ambayo
imepangiwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kukarabati magari na
mitambo iliyokuwa imeharibika na kuacha kufanyakazi kwa muda mrefu,
vitendea kazi ambavyo vinatumika katika kuendeleza sekta ya umwagiliaji.
Hayo
yamesemwa, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.
Daudi Kaale, alipokuwa akizungumza Mjini Dodoma, kuhusu ufufuaji na
ukarabati wa mitambo inayotumika katika ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ya Umwagiliaji.
“tunapojenga Miundombinu ya
umwagiliaji tunahitaji mitambo na magari makubwa, Kwa hivyo inafanyika
kazi kubwa kwasasa yakufufua vitendea kazi hivyo ili kuweza kujenga
uwezo wa Tume na kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji.” Alisema Bw.
Kaali
Aliendelea kusema kuwa vitendea kazi hivyo ni muhimu sana
hasa kwa sasa wakati ambao Tume inakaribia kuanza kutekeleza miradi ya
umwagiliaji kwa kupitia force account.
“Miradi hii ambayo
inategemea kuanza kutekelezwa kupitia force account inategemea kuanza
kutekelezwa mwezi huu hivyo tunahitaji kuwa na vitendea kazi vyakutosha,
na mpaka sasa tumeweza kufufua mitambo iliyopo mikoa ya Mbeya ambapo
kulikuwa na mitamboa mbayo ilikuwa imeharibika tumeweza kuifufua lakini
pia hata hapa makao makuu Dodoma kumekuwa ma mitambomingi, ambayo nayo
pia ilikuwa imeharibika ilikuwa haifanyikazi tumeweza kuifufua tumefufua
mitambo kama miwili kwa hapa Dodoma katika robo hii ya mwaka, lakini
pia tuna maroli matatu,na kule Mbeya tunategemea kufufua eskaveta ambayo
ilikuwa imeharibika tunategemea nayo itaanza kufanya kazi.”Alisisitiza
AidhaBw.
Kaali aliongeza kwa kusema kuwa,kwa upande wa mitambo ambayo ufanisi
wake umeanza kupungua, nayo itafanyiwa matengenezo yaani,mitambo ambayo
imekaa kwa muda mrefu bila kupata matunzo na matengenezo kwa wakati.
“tunatengemea
kumaliza matengenezo hayo ili tuweze kuanza utekelezaji wa miradi ya
force account, ambayo tunategemea kuanza mwezihuu.”
Awali,
Akizungumza kuhusu swala la kukodisha mitambo kwa taasisi ambazo
zinauhitaji, Bw. Kaali ametoa wito kuwa,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
inakodisha mitambo ya umwagiliaji na mitambo mizito ya ujenzi kama vile
Buldoza na Maroli, kwa wadau mbalimbali kama vile mashirika ya umma.
Alieleza pia kwa watu Binafsi na taasisi mbalimbali ilikuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi huku akieleza vipaumbele vya ukodishawaji wa mitambo hiyo,vinatolewakwa wale wanaofanya shughuli za umwagiliaji wanaotaka kuendeleza skimu zao za umwagiliaji.
Post A Comment: