MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akikata utepe kuashiria kupokea madawati 50 kwenye shule ya Msingi Saruji yaliyotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) leo kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian Kihama

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati aliye vaa suti akiwa amekaa kwenye moja ya madawati  50 yaliyotolewa na Tanga Uwasa mara baada ya kuyapokea
MKUU wa wilayaya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo kushoto ni
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian Kihama na Diwani wa Kata ya Maweni Colvas
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad akitoa hotuba yake wakati wa halfa hiyo ya makabadhiano kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akifuatiwa na
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad kulia ni Diwani wa Kata ya Maweni Colvas Joseph
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saruji Hellen Makange  akisoma taarifa ya shule hiyo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Saruji wakiwa wamekalia madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa leo
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Saruji wakiwa wamekalia madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa leo

Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad akipokea cheti cha shukrani kutokana na Msaada huo wa madawati kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa ajili ya kutambua mchango mamlaka hiyo kusaidia sekta ya elimu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mwalimu Lilian
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika makabidhiano hayo

Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa ya makabidhiano hayo.


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga  (Tanga UWASA) leo wamekabidhi msaada wa madawati katika shule ya Msingi Saruji Jijini Tanga na kuwasaidia kuondoa adha ya wanafunzi wa shule hiyo kukaa chini.

Makabidhiano hayo yalifanyika  shuleni hapo na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Tanga Uwasa  Alawi Ahmad Meneja  (kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji)  kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Alawi Ahmad alisema Mamlaka hiyo leo wanatoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya Msingi Saruji iliyopo Kata ya Maweni wenye thamani ya Milioni 4.5.

Awali Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja Tanga Uwasa alisema mchango huo wa madawati ni mwendelezo katika utekelezaji wa mpango wa Mamlaka wa kuchangia sekta ya elimu kwa kuangalia maeneo yenye mahitaji.

Alisema msaada huo ni hatua mojawapo ya Mamlaka hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na  Rais Dkt John Magufuli katika kutoa elimu bure.

Alisema wanategemea madawati hayo yatatumiwa vizuri na kutunzwa ili yaweze kuwanufaisha watoto wengi kwa miaka mingi.

 “Tunapenda kuishukuru Serikali ya wilaya ya Tanga na Halmashauri ya Jiji kwa ushirikiano mkubwa tunaoupata katika kutoa huduma zetu za Maji safi na uondoaji wa maji taka pamoja na utunzaji wa mazingira”Alisema

Alisema kwa kuenzi mchango huo Tanga UWASA imeona kuna haja ya kurejesha shukrani zake kwa jamii na serikali kwa vitendo kwa kuunga mkono juhudi za uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa shule ya msingi Saruji.

“Tanga Uwasa ni Taasisi ya serikali inayosimamia usambazaji wa huduma ya maji safi na uondoshaji maji taka hivyo tunapotoa vifaa hivi tunaomba wanafunzi na wadau wote wakumbuke kwamba ubora wa huduma za maji unatokana na utunzaji wa mazingira”Alisema

“Lakini pia mkumbuke kulipiaji ankra kwa wakati ,ulinzi wa miuondombinu wa maji safi na maji taka na utunzaji mazingira uendelezaji wa rasilimali watu kama ambavyo shule inavyofanya”Alisema

Alisema kutokana na ushirikiano uliopo na wananchi kuimarisha shughuli za usafi wa mazingira Tanga UWASA tunajivunia jiji halina tatizo la milipuko ya magonjwa.

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwashukuru Tanga UWASA kwa msaada ambao wameutoa utakaosaidia kuondosha changamoto ya uhaba wa madawati kwenye shule hiyo.

Alisema kama Taifa chini ya Rais wamefanikiwa sana kuhamaisha watu wafahamu umuhimu wa elimu hali ambayo imepelekea wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto wao shule bila kusukumwa.

Alisema uwepo wa mwamko wa wazazi kujua umuhimu wa elimu hayo ni mafanikio huku akieleza kwamba Serikali peke yake haiwezi kukidhi mahitaji ambayo ni makubwa maana yake inahitaji madarasa zaidi, walimu wengi,vifaa vingi zaidi,na miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kumfanya mtoto asome,

“Lakini kwa bajeti ya serikali pekee haiwezekani kutimiza mahitaji yao kazi ya serikali ambayo imefanywa vziuri na Rais wetu ya kuelimisha na kuhamasisha na sisi tulipo chini tunaendele kuifanya ili iweze kufanikiwa lazima watu wenye mapenzi mwema wajitokeza kushirik katika kutenda”Alisema 

Alisema wanapopata watu mfano wa Tanga UWASA wanaounga mkono jitihada za Rais na chama chake tunapata matumaini kwamba kweli Tanzania mpya sasa inakwenda kujengeka huku akitoa wito kwa wengine kuitika wito huo.

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saruji Hellen Makange alisema msaada huo wa madwati ambao umetolewa na Tanga UWASA utawasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuondokana na tatizo la kukaa chini ambalo wamekuwa nalo .

“Kwa kweli tunashukuru sana kwa msaada huo wa madawati utatusaidia kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa chini ambalo sio nzuri”Alisema Mwalimu hiyo.

Akizungumzia changamoto zilizopo shuleni hapo alisema moja wapo ni kukosekana kwa ulinzi shuleni hapo tatizo ambalo linapelekea baadhi ya shughuli kukwama kutekelezeka kutokana na ulinzi.

“Kwa mfano tunazo kompyuta tangu 2015 ila ni hatari kuzifungia shuleni kwani hakuna uhakika wa usalama  lakini pia kumekuwa na udokozi na uharibifu katika baadhi ya miundombinu ya shule”Alisema

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: