NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais mazingira na muungano Muhandisi Joseph Malongo amesema serikali imeweka mpango mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi utakaoanza mwaka 2021 hadi 2026.
Muhandisi Malongo aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 12 wa taasisiya wahandisi Tanzania uliolenga kuangalia ni jinsi gani wahandisi hao wataendelea kufanya zao bila kuharibu mazingira.
Alieleza kuwa katika mkakati wameweka kipengele ambacho kila sekta inatakiwa kufanya ili kupunguza ukali wa mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwa ni pamoja na kuleta mradi vitakavyosaidia katika suala hilo.
Alifafanua kuwa suala la mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia nzima hivyo wanajitahidi kuongea katika kwenye mikataba ambayo itawasaidia ambapo wamejiunga na jumuiya za mashirikiano Afrika masamhariki na SADC.
" Tanzania imeridhia mikataba mingi ikiwemo mkataba wa Paris unaozungumzia mabadilikoya tabia ya nchi, Mabadiliko ya Kigali unaozungumzia kupunguza gesi inayotumika kwenye viyoyozi ambayo inaleta inaathiri kwenye tabaka la ozon, kuna ya taka hatarishi, kuna ya matumizi ya zebaki na mikataba mingine mingi lakini yote hii inaruhusu nchi zinazoendela kujengewa uwezo,Alisema Muhandisi Malongo.
Aliendelea kusema kuwa ili nchi update nafasi ya kujengwa uwezo ni lazima waandike andiko ambalo linaeleza ni tatizo gani lilo katika nchi yako na baada ya kupata msaada huo nchi yako itanufaika namna gani lakini changamoto iliyopo ni kwamba hatutumia fursa hii na maandiko machache yanayoenda hayakidhi vigezo wanayohitaji wafadhili hao.
Aidha kwasababu ya changamoto hiyo aliwataka wahandisi kuzijua fursa zilizopo katika mikataba mbalimbali na kujenga uwezo wa kuandika maandiko ambayo wataweza kukubalika na wafadhili wa mikataba hiyo.
"Miradi inaandikwa nchi kwa nchi kwahiyo kwanza Injinia anatakiwa kujua ni ni changamoto ili amewataka kuishughulikia kwanza, kama ni mafuriko, kama ni mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri usalama wa chakula, kama ni Katibu maji machafu nakuendelea na wakipita waone kweli tatizo hilo lipo na linahitaji ufumbuzi, Alieleza.
Kwa upande wake rais wa taasisi hiyo Muhandisi Menye David Manga alisema kuwa mkutano huo ni sehemu ya mikutano yao wanaofanya kila mwaka ambapo mwaka huu wanajadiliana juu ya uhandisi endelevu katika mazingira ya tabia ya nchi kwa kujaribu kuangalia kazi wanazozifanya zisiendelee kuharibu mazingira.
"Tutatizama mazingira kwaupande wa kilimo, ujenzi, mafuriki, viwanda na mengineyo na baada tutakuwa na mapendekezo ambayo tutayawasilisha kwa serikali," Alisema Muhandisi Manga
Alisema kama Katibu mkuu alivyowapa changamoto ya kuandika maandiko watalifanyia kazi kwani kazi za wahandisi za kila siku zihusiana na mazingira hivyo kwa njia moja ama nyingine watahakikisha kuwa mazingira hayaendelei kuharibika kutokana na kazi wanazozifanya.
Naye Msajili wa bodi ya wahandisi Patrick Barozi alisema kuwa hadi sasa wana wahandisi 29862 ambapo wana dhamana kubwa ya kutoa huduma za kihandisi kwa manufaa ya jamii na nchi kwa ujumla kwani wapi katika kila sekta ya maendeleo na kijamii.
Alifafanua kuwa endapo ikatokea muhandisi hajatekeleza wajibu wake katika mradi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kusimamishwa na kufutiwa kufanya kazi za uhandisi na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopia zaidi ya wahandisi 364 wameshachukuliwa hatua kwa makosa mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha na kuusimamia vibaya miradi.
Post A Comment: