Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt binilith Mahenge wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt binilith Mahenge katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Mratibu wa Wakala wa barabara za Mjini na Vijijini TARURA, Mhandisi Lusako Kilembe akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt binilith Mahenge katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Mhandisi Frank Chambua akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt binilith Mahenge wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu ya huduma za kijamii katika maeneo hayo.
Meneja wa ufundi kutoka DUWASA Mhandisi Kashilima Mayunga akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt binilith Mahenge wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyoiva kwa ajiri ya uwekezaji na makazi katika jiji la Dodoma na kuangalia utayari wa miondombinu ya huduma za kijamii katika maeneo hayo.
.......................................................................................................
Na Alex Sonna,Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ameziagiza taasisi zinazotoa huduma za kijamii katika Mkoa wa Dodoma zikiwamo TARURA, TANESCO na DUWASA kuandaa mpango maalumu kwa kila taasisi wa kupeleka huduma za kijamii katika maeneo yote yaliyotengwa na jiji kwa uwekezaji na makazi ili kuhamasisha wawekezaji kujitokeza kwa wingi.
Dkt Mahenge ametoa wito huo jijini Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yote yaliyoiva kiuwekezaji na makazi katika maeneo ya Nala, Nala IFM, Mahungu, Michese, Mkalama na Iyumbu katika jiji la Dodoma ambapo amesema wawekezaji wengi hawajitokezi kwa sababu hakuna huduma za kijamii katika maeneo hayo.
“Wawekezaji wanasita kuja kuwekeza katika maeneo haya huduma za kijamii hamna wanahofia kukwama kwa shughuli zao, pia kama unavyoona kuna watu wamejenga majumba mazuri lakini hawana huduma muhimu huku ni kukatishana tama” amesema Dkt Mahenge.
Ametoa mwezi mmoja kwa kila taasisi kuhakikisha inaandaa mpango mahususi na kupeleka katika ofisi yake ya namna kila taasisi ilivyojiandaa kupeleka huduma za kijamii katika maeneo ya uwekezaji na makazi ya wananchi.
“Nataka kila taasisi ije kwangu na mpango imejipangaje kupeleka huduma katika maeneo hayo, kama ni TARURA uje na mpango umejipangaje kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote, kama ni DUWASA umejipangaje maji yapatikane ili tusiwacheleweshe wawekezaji wetu” amesema.
Amezitaka taasisi hizo kuhakikisha zinafanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi kwa wakati, na kuzitaka taasisi hizo kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji na wananchi kukosa huduma hizo za kijamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma Bw. Joseph Mafuru amesema katika eneo la uwekezaji la Nala lina ekari 2713 na tayari wamesha lipa fidia kwa wananchi ya shilingi bilioni 3.5, na eneo linaviwanja 189 kwa ajili ya viwanda na vina ukubwa unaoanzia ekari moja(1) hadi ekari mia mbili na hamsini(250).
Amesema eneo hilo ni zuri kwa wawekezaji kwa sababu limeunganishwa na barabara za mzunguko(ring road) zitakazo lizunguka jiji la Dodoma na tayari wameshaanza kupokea maombi kutoka makampuni mbalimbali yakiwamo ya TBL, Serengeti Browers na wafanyabiashara kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
Aidha ameeleza kuwa kwa maeneo ya makazi tayari wameshapima na wako katika hatua mbalimbali za umilikishwaji na kutoa vibali vya ujenzi katika maeneo mengi ikiwamo maeneo ya Mahungu, Michese, Iyumbu na eneo linalokuwa kwa kasi la Mkalama jirani na chuo kikuu cha Dodoma UDOM.
Post A Comment: