NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta amewataka wataalamu wa manunuzi kutambua katika miradi wanayosimamia waserikali hivyo wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa.
Kimanta aliwaeleza hayo wakati akifunga kongamano la 11 la wataalamu hao ambapo alisema fedha zinazotumika kutekeleza miradi hiyo ni fedha za kodi wananchi na hata ikiwa ni msaada kutoka nje inaletwa kwaajili ya watanzania na mahusiano yaliyopo hivyo akikisheni hamuikwamishi serikali.
"Mnapofanya vibaya watu hawatajenga chuki na nyie bali na mfumo nzima wa serikali na hata kwenye misaada kosa Laki wewe mtu mmoja tu linaweza kuharibu mahusiano ya nchi na nchi,"Alisema Kimanta.
Alieleza kuwa gani ya ununuzi na ugavi ni jukumu lao kuhakikisha nchi inakuwa katika uchumi wa viwanda hivyo wanahitajika wataalamu wenye sifa stahiki, nidhamu ya kazi, uzalendo, maadili na weledi wa hali ya juu.
"Nina imani kuwa mnajua malengo na mikakati ya serikali ya awamu ya tano katika kukuza viwanda na katika kuusimamia hili akikisheni mnatimiza wajibu wenu mnapokuwa katika maeneo yenu ya kazi," Alisisitiza.
Alifafanua kuwa kwa yoyote atakayefanya hilaza kukwamisha juhudi za serikali hatafumbiwa macho wala kuonewa huruma na kwa kuchukuliwa hatua za kisheria na kupewa adhabu itasaidia kuleta nidhamu ya kazi.
Aidha alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya waajiri hapa nchini wanaoajiri watu wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi na haijulikani wanatumia vigezo gani kuwaajiri jambo ambalo kisheria ni kosa kwani anakiuka sheria ya bodi ya ya wataalamu namba 179.
"Ni kosa kubwa kuajiri mtu wa manunuzi na ugavi ambaye hajasajiliwa naagiza bodi mchukue mchukue hatua za kisheria na mnaposimamia sheria msione huruma kwani waliosajiliwa wana vitu vya ziara,"Aliagiza.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa PSPTB Godfrey Mbanyi katika mkutano huo wamejadili jinsi kuusimamia na kuweza kuboresha ili kuweza kufikia ubora wa hali ya juu katika usimamizi wa mnyororo wa manunuzi na ugavi.
"Tulioyajadili tumeyachukua na yawasaidia kuboresha taaluma na taasisi kwa ujumla," Alisema Mbanyi.
Hata hivyo aliwataka wataalamu hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufanikisha nchi katika maendeleo ambayo Rais amekusudia.
Post A Comment: