NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha kwa kuangali utawala bora katika eneo la ununuzi na ugavi.
Akizungumza katika mafunzo hayo kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo Godfrey Mbanyi alisema kuwa lengo ni kujaribu kukumbushana namna bor a ya kuendesha ununuzi hasa kwa kuzingatia bajeti ya serikali inapitia katika mchakato wa ununuzi.
Mbanyi alisema kuwa pia wanajaribu kuangalia namna bora ya kupunguza madhaifu ambayo yanasababisha kupoteza fedha nyingi za umma katika ununuzi na ugavi.
“Mafunzo haya ni mwendelezo wa kazi zetu ambazo zipo kisheria za kuishauri serikali namna bora ya kuendesha michakato ya ununuzi na ugavi ili kujua jinsi taratibu zinavyotakiwa kufanyika na wao kujitadhimini ni wapi walikuwa hawafanyi vizuri,”Alisema Mbanyi.
Mkurugenzi wa fedha na utawala wa Bodi hiyo Paul Belabaye alieleza kuwa wanajadiliana na wataalamu hao ili kujenga uwezo kwenye eneo la ununuzi na ugavi ikiwa ni pamoja na kukumbushana majukumu kila mtu katika eneo lake kwa maana ya zabuni, kamati inayoidhinisha bajeti, kamati ya tathimini,maafisa maduhuri,watumiaji na wadau.
“Katika eneo hiki tunahitaji kuahirikiana ili tuweze kupata thamani bora ya fedha kwasababu ushiriki wa kila mmoja unaleta mtangamano lakini pia kusisitiza utumiaji wa ununuzi wa umma,”Alisema Belabaye.
Alifafanua kuwa mfumo wa TANEPS umeingiza ubora na umeondoa manung'uniko kwani wataalamu hawakutani tena jamii ya wazabuni kutokana na zabuni kutangazwa kwenye mfumo na wazabuni kuomba kupitia mfumo huo.
“Hii imeondoa dhana kwamba wataalamu wanapanga ama kushirikiana na wazabuni kwenye kupanga na pia umechangia kumyima mtaalamu nafasi ya kuamua au kuchagua nani aingie kwenye zabuni,” Alieleza.
Aliendelea kusema kuwa mfumo huo umeongeza uwajibikaji na imani kwa ya wadau kwa wataalamu katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi zaidi.
Alisema kuwa pia watapata utekelezaji wa force account kwenye ununuzi wa umma kwani ni agizo lautekelezaji wa bajeti ya serikali kuhakikish kwamba kazi za ujenzi zinaIngatia utekelezaji wa force account kwa ufanisi.
“Force account ni utaratibu wa ujenzi ambao mwenye jengo ananunua vifaa alafu anamtafuta fundi, anakuja kujenga kupitia vifaa alivyonunua lakini pia unasimamia ubora wa vifaa ulivyonavyo,”Alifafanua.
Alieleza kuwa Dhana hii sasa imekwenda katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa na maeneo mengine ambapo taasisi ya umma inaweza kununua vifaa vya ujenzi, kukodisha mitambo na kusimamia kazi bila kulazimika kuwa na mkandarasi.
Alisema kuwa katika matumizi ya force account yapo ya kuzingatia ambayo ni upatikanaji wa vifaa vya ujenzi, upatikanaji wa wataalamu ambao wanafanya kazi kubwa katika ngazi ya jamii na walikuwa hawapati nafasi ya kujenga taifa katika sekta hii ya ununuzi wa umma kwasababu walikuwa wanaonekana hawana uwezo wa kuwa na makampuni.
“Lakini sasa tumejielekeza zaidi kwenye miongozo inayoeleza usimamizi, kwa maana ya kamati za usimamizi, kamati ya kupokea na kukagua vifaa lakini pia bodi inasisitiza utunzaji wa vifaa,” Alisema.
Alisema lengo juu ni kushirikiana na wataalamu wengine kuhakikisha kuwa wanaboresha mazuri ambayo tayari yameshaonekana kwenye force account ili kuweza kuisaidia serikali kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
Alieleza kuwa mikataba ya ununuzi ina mambo matatu ya kuzingatia ambayo ni lazima usimamie ubora wa jengo na vifaa vinavyotumika, umalizaji wa jengo kwa wakati pamoja na gharama na mwiaho wa siku jamii ielewe kuwa unapotumia force account unaokoa fedha kwa kuhakikisha mikataba inaonyesha usimamizi wa fedha
Post A Comment: