Mwenyekiti wa chama cha Wataalamu Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) Dkt. Daniel Komwihangilo akitoa salamu za chama hicho wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Imebainishwa kuwa kadri watu wanaokaa mijini vipato vyao vinavyozidi kukua na kuongezeka ndivyo matumizi na mahitaji ya mazao ya mifugo na uvuvi yanavyoongezaka hivyo uzalishaji wa mifugo na samaki lazima uboreshwe ili kukidhi mahitaji hayo.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Profesa. Elisante Ole Gabriel kwa niaba yake na Mkurugenzi wa wa sera na mipango wa Wizara hiyo Amosy Zephania wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 43 la uzalishaji na uendelezaji wa mifugo na mkutano wa 44 wa mwaka wa chama cha Wataalamu wa uzalishaji na uendelezaji wa mifugo Tanzania (TSAP)kilichofanyika Jijini Dodoma.
Alisema kuwa Mahitaji ya lishe na protini inayotokana na Mifugo yanatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka 20 ijayo kutokana na ongezeko la watu,kukua kwa miji na kuongezeka kwa kipato cha watu hivyo ni wakati muafaka sasa kufanya mapinduzi makubwa katika uzalishaji na minyororo ya thamani ya mifugo na samaki ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda pia.
" Hapa nchini kwetu uzalishaji wa mazao ya Mifugo haukui kwa viwango vinavyotakiwa kama yalivyo mahitaji ya walaji,hii inaleta umuhimu wa kufanya mabadiliko katika mifumo yetu na kuongeza ufanisi na tija ya uzalishaji kwa kutumia sayansi na teknolojia za kisasa" Alisema Profesa. Elisante.
Katibu Mkuu huyo alisema mifumo ya uzalishajiwa Mifugo na Uvuvi nchini imeegemea zaidi kwenye uzalishaji kwa njia ya mifumo ya asili ambapo Wazalishaji wengi ni Wafugaji na Wavuvi wadogowadogo na mifumo mingi iliyopo bado ni ya asili yenye viwango vidogo na hairidhishi.
Alieleza kuwa kuna haja ya kuongeza upatikanaji wa malighafi zinazotakiwa katika viwanda vya kusindika mazao ya Mifugo na Uvuvi na kuhimiza Wafugaji na wazalishaji kuwekeza katika teknolojia na vitendea kazi sahihi vitakavyoongeza uzalishaji mashambani na kuwezesha kufikia masoko kwa ufanisi zaidi.
"Ninayasema haya yote nikiwa na nia ya dhati kwamba sekta ya Mifugo na Uvuvi bado zina changamoto nyingi na nyinyi Wataalamu na wadau lazima muone ulazima wa kuzikabili na kuzitafutia suluhu na changamoto nyingine nizigusie tuu ambazo ni uharibifu wa ardhi kutokana na mmomonyoko pamoja na mahitaji ya maji safi ya kunywa kwaajili ya mifugo sambamba na mahitaji ya malisho bora na ya kutosha" Alisisitiza Profesa. Elisante.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kongamano hilo Mwenyekiti wa wa chama cha wataalamu wa uzalishaji na uendelezaji wa Mifugo Tanzania (TSAP) kt. Daniel Komwihangilo lisema kuwa chama chao kinaona ni wakati muafaka sasa wa Serikali kutunga sheria ambayo itadumisha udhibiti na usimamizi wa mazoezi halali ya sayansi ya wanyama na kazi ya uzalishaji kama ambavyo ilivyo kwa vyama vingine kama Wahandisi,Wanasheria na wengine wengi.
Alifafanua kuwa kupitia sheria hiyo wataalamu wa sayansi za wanyama na uzalishaji watakuwa na Mdhibiti/Msajili ambaye atahakikisha wataalamu hao wanafuata na kutii sheria na hivyo kulinda maslahi ya Mfugo,Wafugaji na wadau wengine.
Alifafanua kuwa Mda kuu ya mkutano huo wa kisayansi wa 43 ni kuinua viwango vya minyororo ya thamani ya Mifugo na Uvuvi kwa mafanikio endelevu kijamii na kiuchumi lakini kuna mada nyingine ndogo nyingi ambazo zimejikita kwenye maeneo mahususi ya ukuaji wa teknolojia na matumizi ya yake katika kuboresha wa Mifugo na viumbe maji pamoja na matumizi yake katika uzalishaji bora,ufugaji na sera.
"Ni nafasi sasa kwa wizara husika inayoshughulikia maendeleo ya Mifugo nchini kuchukua hatua hii na sisi kama TSAP tupo tayari kutoa ushrikiano wowote utakaohitajika katika jitihada hizi" Alisema Dkt. Komwihangilo.
Dkt. Komwihangilo amesema TSAP wameomba eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 7680 kwenye jiji la Dodoma ambalo wanaamini wataliendeleza kwaajili ya kusaidias kutoa huduma za ushauri kwa Wafugaji,Wanafunzi na wadau wengine kirahisi hivyo wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 36,827,674 kulinunua.
Post A Comment: