MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Songea , MICHAEL Mbano ameupongeza Umoja wa Waandishi wa Habari wanawake (WJ) nchini ambao wameguswa na kumkabidhi Cherehani na fedha sh.50000 Binti Gonzalva Rungu (19) aliyezaliwa akiwa hana mikono na mguu mmoja.
Mlemavu huyo ni mhitimu wa kozi ya ushonaji katika chuo cha ufundi stadi VETA kilichopo Mkoani Ruvuma ambaye ni mama mtoto mmoja .
Akikabidhi Cherehani hiyo jana wakati wa mahafari ya 35 ya chuo cha (VETA Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Mkoani Ruvuma , Joyce Joliga
Joliga alikabidhi Cherehani pamoja na fedha kwa niaba ya wana umoja huo na kisha Mstahiki Meya mteule wa Manispaa ya Songea kumkabidhi Mlemavu huyo .
Mhe.Mbano alisema,amefurahishwa na kitendo cha waandishi hao kuguswa na kujitoa kwa watu wenye ulemavu kwani wameonyesha utu na ameahidi kuunga mkono kwa kutoa sh 500,000 ili kuweza kumsaidia Gonzalva pamoja Mlemavu wa kiume ambaye hana mikono wala miguu Ridhiki Ndumba.
Alisema,Waandishi wa habari wamekuwa msaada kwa jamii kwa kuibua na kuandika habari za maendeleo ambapo amewataka wananchi kushirikiana nao na kupeleka watoto wenye ulemavu chuoni kwani wanayo haki ya kupata elimu na kupata ujuzi wa mbalimbali.
Aidha, Meya huyo amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumsaidia binti huyo shilingi milioni tano ambazo zimemsaidia kupata kiwanja na makazi ya kudumu ya kuishi .
"Niwapongeze sana waandishi wa habari wanawake mlioguswa na kujichangisha kidogo kidogo na kisha kuja na wazo la kumsaidia mdogo wenu kwa kumnunulia mashine ya kushonea nguo, mmefanya jambo kubwa na zuri, mbarikiwe sana na muendelee kuibua na kusaidia wananchi nasi tunaendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ,nawaunga mkono nami nitatoa sh 500,000 ili ziwasaidie ndugu zetu hawa wawili Gonzalva na Ridhiki,"alisema Mbano.
Awali Mkuu wa Chuo cha VETA Songea , Gideon Ole lairumbe aliwashukuru Waandishi hao kwa kuweza kumwezesha binti huyo kwani itamsaidia kuweza kuanza kufanya kazi ya ushonaji na kujiingizia kipato cha kujikimu yeye na mwanaye.
Alisema, waandishi wameonyesha Moyo wa kipekee na kuwataka wasiache kwenda chuoni hapo kwenda kuandika habari mbalimbali za kuwasaidia wananchi ikiwemo za kozi zinazotolewa chuoni hapo.
Naye Mwenyekiti wa Umoja huo Esther Macha ameelezea kuwa Wazo la kumchangia mlemavu huyo lilipelekwa na Joyce Joliga mwandishi wa gazeti la Mwananchi Songea ambaye aliibua habari hiyo kwa kumwandikia makala binti huyo.
Alisema waandishi wa habari waliguswa na kuamua kumchangia mhitimu huyo baada ya kuweka picha ya mlemavu huyo status ambapo alikuwa akiombwa ahudhurie mahafari yake na aende na zawadi na Joyce aliahidi kumsaidia kwa kuweka status kwenye simu yake ili watakaoguswa wamsaidie kwani mara kwa mara mara amekuwa akimsaidia kwa mahitaji madogo madogo ya kibinadamu kama mdogo wake.
“Tunamshukuru sana Mwezetu Joyce Joliga kwa kuibua habari ya binti huyu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akimsaidia kununua mahitaji ya chuo na kumpa mahitaji ya kulea mwanae”alisema Macha
Hata hivyo baada ya picha kuwekwa baadhi ya waandishi akiwemo Afisa Habari wa Wizara ya Afya Bi. Catherine Sungura ambaye pia ni Mwekahazina wa umoja huo aliwaomba waandishi wa habari kujitoa kwa chochote kama kawaida yao na kumchangia zawadi kubwa ili iwe ukumbusho wake kama alivyoomba.
Post A Comment: