Mbunge wa Viti Malum Mkoa Kaskazini Unguja Bi Angelina Malembeka (Kulia)  akiwa na Afisa Mazingira wa Wilaya Kaskazini B (kushoto) Mashavu Khatib ,  wakati wa kugawa majiko ya gesi 130 kwa wanawake wa mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka (Kushoto) akikabidhi majiko Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Kaskazini Unguja Maryam Muharam Shomari leo ukumbi wa CCM mkoa  Zanzibar ambapo Malembeka ametoa majiko 130 kwa wanawake  (kushoto) Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja  Rajabu Ally Rajabu (PICHA NA HERI SHAABAN)

 NA HERI SHAABAN (ZANZIBAR) 


MBUNGE wa Mkoa Kaskazini Unguja Bi.  Angelina Malembeka,leo amegawa majiko ya gesi kwa wanawake wa Mkoa  wa Kaskazini Unguja pamoja na kuwapa elimu ya utunzaji wa Mazingira.


Dhumuni la kugawa majiko hayo kuzuia ukataji miti, na uhamasishaji wa  matumizi ya  gesi ambayo  inapatikana katika mkoa huo   wa  Kasikazini Unguja ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya utunzaji mazingira na  nishati  ya gesi inayopatikana Mkoani  humo.


Akizungumza  katika semina hiyo ya Mazingira Mbunge Malembeka alisema

anakipongeza Chama cha Mapinduzi kwa ushindi mnono Tanzania Bara na visiwani  pamoja na Wanawake kukiletea ushindi Chama cha Mapinduzi CCM. 


" Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaimiza katika suala la utunzaji mazingira  na  hutumiaji  na gesi,nakabidhi majiko ya gesi kwa Wanawake wa mkoa huu ili watumie katika shughuli zao nyumbani na kwenye  ujasiliamali wao, pia wawe mabalozi wa kutunza mazingira wasikate miti kwani ni vyanzo vya maji " alisema Malembeka.


Aliwataka Wanawake wa Kaskazini Unguja kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali   katika kujikwamua kiuchumi, kutumia majiko ya gesi vizuri kwa sasa yameboreshwa hayana madhara kwa matumizi nyumbani. 



Aliwataka waunge mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar  pamoja na Chama cha Mapinduzi pia wawe chachu ya maendeleo 



Aidha aliwataka wanawake wa mkoa huo kushirikiana kwa pamoja katika kazi za maendeleo  na uzalishaji kiuchumi ili waweze kusonga mbele kwani wanawake wanaweza.



Kwa upande wake mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Kaskazini B  Rajabu Ally Rajabu alimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu Angelina Malembeka kwa kuwawezesha majiko ya gesi Wanawake 130 wa mkoa huo na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano. 


Mkuu wa Wilaya Rajabu alitumia nafasi hiyo kupongeza chama cha Mapinduzi CCM kwa ushindi pamoja na Mbunge Malembeka kuwakumbuka wapiga kura wake  ikiwemo kutatua changamoto za Wanawake kila wakati .


Aliwataka watunze Mazingira kila wakati

na kuzingatia usafi kwani ndio utamaduni .


Alisema wameweka utaratibu eneo la Kiwengwa kuzindua usafi   

Pia wataweka sheria ya wachafuzi wa mazingira na watakaochafua mazingira watakamatwa. 


Alisema majiko ya gesi kwa matumizi nyumbani yanarahishisha pia gharama ndogo amewataka wayatunze vizuri waache kukata miti ovyo Mkoa Kaskazini Unguja. 



 Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa  Maryam Maharam Shomari ameomba serikali iwatengee eneo kwa ajili ya dampo maalum wawe wanatupa taka wananchi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: