Na Woinde Shizza ,ARUSHA 


Kampuni ya kutengeneza Pikipiki ya Keeway Motor, imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuidhamini klabu ya soka ya Nyota ya jijini Arusha.


Akiongea wakati wa kungia mkata na timu hiyo Msimamizi mkuu wa tawi la kampuni ya Keeway mkoani Arusha ,Lydia Kaguru  alisema kuwa wameamua kuidhamini timu ikiwa  ni njia moja wapo ya kuinua vipaji vya vijana.


Alisema wameingia Mkataba wa mwaka mmoja kuidhamini timu hiyo na kila mwaka wanatarajia kutumia shilingi milioni 10 ,na Mkataba huo unaanza kufanya kazi January moja 2021,lakini kwakuwa wameshaingia Mkataba wameanza kuwapa vitu mbalimbali Kama jezi.


"Kampuni yetu aijaanza kudhamini michezo hapa bali  ,inasaidia timu mbalimbali Katika kila eneo ambalo tunatoa huduma ambapo sisi Kama sisi tunatengeneza pikipiki hizi pamoja na spea za pikipiki na tumezagaa katika nchi 85 duniani  ikiwemo hapa Tanzania "alisema Kaguru


Alisema mbali na kudhamini pia wachezaji na mashabiki watapata nafasi za kujaribu na kutumia pikipiki zao bila malipo yoyote endapo watakuwa na uhitaji wowote wa usafiri. 


Kwa upande wake Meneja wa timu ya  Nyota  Thobias Julius alishukuru kwa udhamini huo na kubainisha kuwa timu hiyo awali ilikuwa ikipitiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukosa nauli za wachezaji za kwenda kwenye mechi,jezi pamoja na vitu mbalimbali .


Alisema kuwa msaada huo umekuja mda muhafaka kwani utawasaidia kupata nauli ,jezi  hasa Katika kipindi hichi ambacho timu yao iliopo ligi ya mkoa kufanya vizuri Katika zilizobaki kumaliza mzunguko wa ligi


Akizungumzia msaada huo  kaimu katibu Chama Cha mpira wa miguu mkoa wa Arusha Emanuel Antoni  alisema kuwa wamepata faraja kuona kunawadhamini wanajitokeza kudhamini timu za ligi za Chini pamoja na zile za mchamgani.


Aliwataka wasiishie  kuidhamini timu hiyo bali wadhamini na timu nyingine kubwa za mkoani Arusha ambazo zipo Katika nafasi za juu Kama  AFC iliopo ligi daraja la kwanza pamoja na zingine.


Naye nahodha wa timu hiyo aliwahaidi wadhamini hao kufanya vizuri na kusema kuwa wanawahaidi hawaja waangusha.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: