NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wametakiwa kuhakikisha elimu wanayotoa inawasaidia vijana kuwa wabunifu na wavumbuzi ili kuweza kujiajiri na kuajiri wengine kwa lengo la kupunguza idadi ya ukosefu wa ajira nchini.
Hayo yaliasemwa na Askofu wa jimbo kuu katoliki la Mbulu,Antony Lagwen wakati akizunguza katika mahafali ya nne ya chuo cha St.Augustine tawi la Arusha ambapo alisema kuwa ubunifu ni matokeo ya kufikirisha ubongo ili kuibua njia mpya katika kuleta mabadiliko au kutatua changamoto zinazoikumba jamii katika nyanja zote za maisha.
"Pamoja nakuwaandaa wahitimu ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine mnapaswa kuwafundisha na kuwatayarisha kuwa wabunifu na kuondokana na dhana ya kwamba ubunifu ni kitu alichozaliwa nacho mtu kwani kitendo hicho ni katika kusoma na kujifunza kiustadi na kuongeza bidii,"alisema Askofu.
Askofu Lagwen aliwaeleza waadhiri kuwaongoze vijana vyuoni kufanya tafiti zenye tija kama fursa za kutatua changamoto za maisha ikiwa wakati huohuo wakiweza kujiajri na kuajiri wengine kwa lengo la kukabiliana na mazingira yatakayomsaidia kuondokana na utegemezi pamoja na vitu hivyo kuwa dira ya utoaji elimu vyuoni.
"Kama waadhiri mnapaswa kuwajengea ujasiri wa uthubutu na kuachana na mazoe ya utoaji maelekezo wakati wote na kuwapangia vijana nini cha kufanya nakutoa mafunzo ambayo yatawasaidia kuwa wabunifu kwani biashara nyingi zinayumba na kufa kutokana na kukosa ubunifu kwa maana hiyo kukosa ubunifu ni hatari sana kwa mfanyabiashara au taasisi yoyote kubaki katika ushindani," Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa chuo hicho Padre Charlse Gervason alisema wahitimu 305 walipaswa kuhitimu chuo lakini kutokana na sababu za kitaaluma,kijamii na kiuchumi wanaojitimu ni 256 na kati ya hao wakiume ni 170 na wakike ni 135 na jumla ya wahitimu 10 walitunukiwa vyeti ikiwa nane walipata ufaulu wa daraja la kwanza.
Mkurugenzi huyo alisema anashukuru Mungu kuwa baadhi ya vijana wanaohitimu wameshajiajiri na kuajiri wengine kwa kufungua makampuni yao ya utalii hivyo ni wito wao kwa wahitimu kuendeleza ubunifu ili wakaitumikie taifa na serikali inamchango mkubwa katika elimu ya juu kwani kati ya wanafunzi 350 wa.shahada ya kwanza 250 ni wanufaika mikopo inayotolewa na Serikali.
"Idadi hiyo ni sawa na asilimia 76.7 ya utoaji mikopo kwa wanafunzi wa chuo hicho kwa mwaka wa kwanza ikiwa wito wetu kwa wanufaika wa mikopo kama hawajaripoti vyuoni kuripoti haraka iwezekanavyo kwani mwaka wa masomo 2020/2021 umeshaanza rasmi hivyo tunaendelea kuishukuru serikali pamoja na watendaji wake wote kwa kutoa mikopo kwa wakati ili wanafunzi waweze kusoma kwa utulivu.
Nawaasa wanafunzi wote walionufaika na mikopo na wengine wetu waliosomeshwa na wazazi pamoja na walezi kuwa kutumia muda wao kujifunza zaidi na kuendeleza yale yote waliofunzwa vyuoni na kuacha kukata tamaa katika kuleta maendeleo binafsi na kwa Taifa.
kwa upande wake mmoja wa wahitimu wa chuo hicho Adam Agrey alisema elimu aliyopata ataenda ataitumia kuibadilisha jamii kupitia nyanja zote na kutumia vyema rasilimali mbalimbali kujiingizia kipato na kuweza kuajiri wengine.
Post A Comment: