Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amewataka Madiwani waliochaguliwa katika wilaya hiyo kuwatumikia wananchi kwa muda wa miaka mitano kwa nguvu zao zote kama walivyoaminiwa na kuchaguliwa
Ole Sabaya ameyasema hayo leo, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa madiwani 24 wa Jimbo la Hai.
Ole Sabaya alizungumza na madiwani hao kwa mara ya kwanza, kuchaguliwa kwake kubwa Mkuu wa Wilaya hiyo.
Amesema kwamba endapo madiwani hao awatafanya kazi ipasavyo hatosita kuwashtaki kwa wananchi kwa maana kazi kubwa ya madiwani ni kutatua kero za wananchi na si vinginevyo.
Sabaya amewataka madiwani kuwaeshimu watendaji wa kata na kushirikiana kwa pamoja kutatua kero za wananchi na pale wanapokwama watafuata taratibu za kufikisha Ofisini kwake na kuzifanyia kazi
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya amesema eshma kubwa ya madiwani pamoja na mbunge ni kuwatumikia wananchi kutatua kero zao na sio namna nyingine kwani matatizo ya watu yakifanyiwa kazi basi esabu yao inakamilika kwa asilimia mia moja
Akizungumzia kero za wananchi hao, Ole Sabaya amesema kuna tabia ya viongozi kunyanyasa watu wa chini kwa kutumia pesa zao lakini sasa basi imekoma kwani wananchi wamekua wakitapeliwa na kukosa haki yako
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai ole Sabaya amevunja mabaraza ya ardhi, baada ya kutumika kisiasa kunyanyasa wananchi wanapo peleka malalamiko ya migogoro ya aridhi
Amemwagiza Mwanasheria wa Halmashauri ya Hai, Blandina Mweta kuvunja mabaraza ayo kwani yamekua ya wapiga dili kunyanyasa wananchi nakushindwa kutatua kero zao na kuchagua mabaraza mapya ya aridhi.
Ole Sabaya amemwagiza pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai, Yohana Sintoo, kuwapa ushirikiano madiwani pamoja na kuwakutanisha watalaam wake kufanya kazi changamoto za kata wanazo toka lengo ikiwa kufanya kazi kwa kushirikiano na kwa pamoja
Nimeanza kusikia huko nje watu wanaulizana kuwa kati ya Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri ni nani mkubwa, acha ni seme kwamba atakaye kuwa mkubwa kati ya Mwenyekiti na Mbunge ni yule ambaye atafanya kazi kubwa ya kutatua kero za wananchi na kuongeza mapato ya halmashauri.
Zaidi alisisitiza kuwa na yule atakaye tatua kero za wananchi ikiwemo bara bara Maji safi na salama pamoja na changamoto zote ambazo zinawakabili wananchi fanyeni kazi za kutumikia wananchi zitawafanya kua wakubwa na sio kujinua alisema Sabaya
Amesisitiza kua viongozi waliochaguliwa hasa Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri kuna watu wanawashindanisha kuwa ni nani mkubwa kati yao.
Aidha, Ole Sabaya amewaeleza kuwa ukubwa wa kiongozi unapimwa mwingine kwa kazi na sio vinginevyo hivyo wananchi watapima aliyekua mkubwa kati ya mwenzake ni nani aliye waletea maendeleo na sio longolongo
Mwisho
Post A Comment: