Wananchi wa Kijiji cha Bweni wilayani Pangani ambacho kimefanya vizuri katika Shindano ya Mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia zidi ya Wanawake na Watoto wakiwa na tuzo yao huku wakisheherekea baada ya kuibuka na ushindi wa Vijiji ambavyo vimefanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wilayani Pangani
Wananchi wa Kijiji cha Bweni wilayani Pangani ambacho kimefanya vizuri katika Shindano ya Mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia zidi ya Wanawake na Watoto wakiwa na tuzo yao huku wakisheherekea baada ya kuibuka na ushindi wa Vijiji ambavyo vimefanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wilayani Pangani
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia akitoa tuzo kwa mmoja wa viongozi wa vijiji vilivyofanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto wilayani humo.

Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza mjini humo wakati wa tamasha la kuwazawadiwa vijiji bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo lililoendeshwa na Shirika la Uzikwasa wilayani humo kulia ni Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa
ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza mjini humo  wakati wa tamasha la kuwazawadiwa vijiji bora katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo lililoendeshwa na Shirika la Uzikwasa wilayani humo kulia ni Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa

 

SERIKALI wilayani Pangani mkoani Tanga imeitaka jamii kutoyaficha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na Watoto kwani kwa kufanya hivyo wanachangia kurudisha nyuma jitihada za maendeleo katika Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mwalimu Hassani Nyange wakati wa tamasha la kizawadia Vijiji vilivyofanya vizuri katika mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na Watoto wilayani humo.

Alisema Kuwa swala la ukatili wa kijinsia katika jamii ni tatizo ambalo Kama halitatolewa taarifa  na hatua za kisheria kuchukuwa mkondo wake litaendelea kuleta athari zaidi .

"Hivi vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto wadogo Kama kubakwa na kulatiwi ndio ikiwa havitadhibitiwa kwa haraka vitaweza kuleta athari zaidi kwa watoto hao ambao ni Taifa la kesho"alisema DAS Nyange.

Nae Mratibu wa tamasha hilo kutoka Shirika la Uzikwasa Salvata Katanga alisema kuwa Shirika hilo limekuwa likiwazawadia tuzo Vijiji kumi ambavyo vinafanya juhudi kubwa katika kupinga mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani humo.

Alisema kuwa tamasha hilo limeweza kusaidia viongozi wa Vijiji husika kuwa wabunifu katika kudhibiti vitendo vya ujanyanyasaji kwa kutoa taarifa mapema katika vyombo vya usalama na hatua kuchukuliwa.

Kwa upande wao  baadhi ya viongozi wa Vijiji walisema kuwa elimu waliyoipata imewezesha kusaidia kuishirikisha jamii katika utekelezaji wa mpango Kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mkwaja Saleh Mwinjuma alisema kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya athari za ukatili na namna ya kuripoti matukio hayo kwenye vyombo vya kisheria

"Elimu imesaidia kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia kwani hapoa awali wananchi walikuwa wanaogopa kutoa taarifa lakini baada ya kupata elimu sasa jamii imehamasika kutoa taarifa hizo"alisema Mwinjuma.

Nae Mwakilishi wa dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi Ismail Ali alisema kuwa kutoka na jamii kuhamasika hivi karibuni waliweza kupa taarifa ya matukio ya watoto kulawitiwa na waliweza kufanikiwa kuwatia nguvuni wahusika.

"Hivi karibuni tulipata taarifa ya watoto watano kulawitiwa katika kata ya Boza na kutokana na ushirikiano wa jamii tuliweza kuwatia nguvuni wahusika na Sasa wanatarajia kufikishwa Mahakama  wakati wowote"alisema Ali.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: