Na Vumilia Kondo- Morogoro

Imeelezwa kuwa Ili wananchi wanufaike na faida mbalimbali zinazotokana na misitu ya vijiji inapaswa sera ,sheria ,kwanini na matangazo ya Serikali (GNs) zinazotungwa ziwe na mlebfo huo na kuhakikisha vikwazo vyovyote vinatolewa.


Hayo yameelezwa katika warsha na mkutano Mkuu wa 20 wa Mtandao wa jamii wa utunzaji misitu (MJUMITA) unaofanyika mkoani Morogoro.

 Bi Nanjiva Nzunda  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo akimuakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro amesema Serikali inafahamu wazi kuwa rasilimali misitu ni muhimu kwa Uchumi wa Taifa na kwa ajili ya kufanikisha sita ya Taifa ya maendeleo.


"Ni wazi kwamba sera,sheria na kwanini pamoja na muongozo inatambua kwamba kijiji kinaweza kutumia mazao ya misitu yao kibiashara Ili kuleta kipato kwa wananchi wa kijiji husika kwa hiyo ni vyema biashara hizi zikawekewa taratibu na muongozo ya kibiashara na tutaona maendeleo makubwa Sana nchini" Alisema.


Ameongeza kuwa kila mwaka Tanzania inapoteza hekta 460,000 za misitu ambapi hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa Ili kunusuru misitu.

"kwa kurasimisha misitu ya hifadhi ya vijiji kutachangia kupunguza ufyekaji hovyo wa misitu hii,kwamfano kutazuia Uvamizi wa misitu kwa ajili ya upanuzi wa mashamba ndani ya misitu,uendelezaji wa Makazi ndani ya misitu,moto,uvunaji haramu wa magogo,uchungaji wa mifugo ndani ya misitu,uchomaji mkaa usio endelevu pamoja na shughuli nyingine za kibinadamuzinazohatarisha usalama wa misitu"Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MJUMITA Bwana Revocatus Njau amesema MJUMITA kwa kushirikiana na Shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania (TFCG) imewezesha misitu 51 kurasimishwa kwa kutangazwa kwenye gazeti la Serikali namba 487 na gazeti namba 688.

Njau Alisema kuwa MJUMITA imeweza kuleta pamoja takribani wanachama 15000 katika usimamizi wa misitu ya asili ya vijiji wakisimamia zaidi ya hekta1,800,0000 katika vijiji 452.

"MJUMITA imeweza kuboresha Maisha ya jamii kupitia shughuli Kama za ufugaji nyuki,kilimo hifadhi,mradi ya maji,ufugaji wa vipepeo,uzalishaji wa mkaa endelevu na uanzishwaji wa vicoba pia kufanikisha uanzishwaji wa nipango ya matumizi Bora ya aridhi kwenye zaidi ya vijiji 40 huko Kilosa,Lindi,Liwale,Nachingwea, Handeni na Mvomero".Alisema

Naye Mkurugenzi msaidizi wa TFCG Emanuel Lyimo amesema suluhisho la kupambana na uharibifu wa misitu ni kutumia njia ya usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii kwa wananchi kuwajibika na kupanga na kusimamia mapato yanayotokana na misitu hiyo.

"Zaidi ya vijiji 1200 ndio pekee vinashiriki usimamizi shirikishi wa misitu na katika vijiji hivi Misitu hekta milioni mbili ndio zimehifadhiwa huku hekta milioni 20 zinapotea bila kuhifadhiwa kwa hiyo tusipokuwa makini tunaupoteza misitu hii". Alisema.

MJUMITA ni chombocha kitaifa ambacho kinaunganisha jamii zinazoishi kandokando ya misitu ya asili na kuwa na sauti ya pamoja juu ya usimamizi wa Misitu na Utawala Bora.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: