Naibu Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Richard Kangalawe amesema Chuo kimekuwa na mchango mkubwa katika Taifa ikiwa ni pamoja na kutoa wataalamu, wabunifu, pia Chuo kimekuwa kikitoa ushauri wa kitaalamu lengo likiwa ni  kuchangia maendeleo katika Taifa. 


Prof. Kangalawe amesema hayo wakati anafungua kusanyiko la siku moja la wanafunzi linalofanyika Chuoni hapo.



Mwenyekiti wa kusanyiko la wanafunzi hao Simon Simalenga amesema wanafunzi wanaosoma katika chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wasijuchukulie poa, kwa sababu wapo Marais ambao wanaongoza nchi mbalimbali za Afrika ambao walisoma katika Chuo hiki”. alisisitiza Simalenga



“ Wahitimu naomba msijuchukulie poa, maana nyinyi ni viongozi wa baadae na hii inatokana na kuwa wapo Marais katika nchi za Afrika ambao walisoma hapa na leo hii ni Marais, 


Kwa upande wake katibu  wa kusanyiko hilo la wahitimu John  Muruga amesema sehemu yeyote utakayokwenda na kukuta mwanafunzi aliyesoma katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anajulikana kwa maadili na Uongozi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: