Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umekutana na wadau inaofanya nao kazi katika kutetea haki za wanawake na wasichana ili kufanya tafakuri ya Mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania unaotekelezwa katika mikoa 9 nchini Tanzania kwa lengo la kukuza usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.

Kikao hicho cha Tafakuri ya Mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi kimefanyika leo Jumamosi Novemba 21, 2020 Jijini Mbeya kwa kuwakutanisha pamoja wanufaika wa mradi kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa na wadau wanaotetea haki za wanawake na wasichana, Wafeminia vijana na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika hlashauri ambako mradi unatekelezwa.

 Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana amesema lengo la kikao hicho ni kujifunza na kushirikishana fursa, uzoefu na changamoto wanazozipata katika kutetea haki za wanawake na wasichana kupitia Mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania.

“Mradi  huu wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania unaotekelezwa na TGNP kwa ufadhili wa  serikali ya Canada (Global Affairs Canada) kwa kipindi cha miaka mitano 2019 – 2024 unaotekelezwa na TGNP kwa ufadhili wa  serikali ya Canada (Global Affairs Canada) lengo likiwa ni kukuza usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana”, amesema Mayumana.

“Mradi huu unalenga kuongeza ushirikiano na ujenzi wa nguvu ya pamoja ili wanawake na wasichana wafurahie maisha na kuongeza usawa wa kijinsia katika jamii”, ameongeza Mayumana.

Amesema mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Mara, Dodoma, Kilimanjaro, Morogoro, Shinyanga, Kigoma na Mbeya.

 “Kupitia mradi huu tunataka wanawake na wadau wa haki za wanawake na watoto wafanye kazi kwa pamoja ‘wajenge TAPO kwa pamoja’  ili kuwa na sauti ya pamoja kuhusu masuala ya wanawake na wasichana itakayowezesha kuwa na sheria na sera rafiki kwa wanawake na wasichana”, amesema Mayumana.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE ACP linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto, John Myola amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto ili iwe rahisi kujua changamoto zao na kuepuka kuwaita majina yasiyofaa.

Pia Myola amewakumbusha wazazi kuwa makini na watu wanaokaa na watoto kwani baadhi yao siyo wema wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya ukatili watoto ikiwemo kuwabaka na kuwapa ujauzito.

“Watoto wetu wanafanyiwa ukatili na kubakwa na watu wa karibu kabisa  wakiwemo wajomba, mashemeji, kaka na baba wadogo na wakubwa. ukiwa karibu na mtoto wako atakueleza matendo anayofanyiwa lakini kama haupo karibu naye, unatumia lugha mbaya kamwe mtoto huyo hatakueleza yanayomsibu”, ameongeza Myola.

Naye Beatrice Yohana Kimambo kutoka Kilimanjaro amewataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano katika kesi za matukio ya ukatili dhidi ya watoto badala ya kuendekeza rushwa ili kuzima kesi hizo.

Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joseph Swalala ameishukuru TGNP kwa kutoa mafunzo kwenye vituo vya taarifa na maarifa ambapo sasa vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia mara tu yanapotokea.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana ili kufanya tafakuri ya mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania unaotekelezwa katika mikoa 9 nchini Tanzania kwa lengo la kukuza usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana leo Jijini Mbeya. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.

Afisa Mkuu wa Programu wa TGNP, Shakila Mayumana akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Mratibu wa Mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania , Flora Ndaba akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Mratibu wa Mradi wa TAPO: Sauti ya Wanawake na Uongozi-Tanzania , Flora Ndaba akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Meneja wa Fedha TGNP, Mwangoa Altho akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE ACP, John Myola akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Mdau wa Haki za wanawake na wasichana Beatrice Yohana kutoka mkoani Kilimanjaro akizungumza katika kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.
Wadau wa haki za wanawake na wasichana wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea.
Wadau wa haki za wanawake na wasichana wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na wasichana wakiwa ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na wasichana wakiwa kwenye kikao cha wadau wanaofanya kazi na TGNP katika kutetea haki za wanawake na wasichana.

 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share To:

msumbanews

Post A Comment: