Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya hati za utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN Credentials Committee) New York Marekani kwa mwaka 2020/2021.
Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika nafasi ya kuongoza kamati hiyo nyeti ya Umoja wa Mataifa ambapo uteuzi wake ulipendekezwa na Ofisi ya Rais wa Baraka Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kwa kauli moja na wajumbe wote tisa wa Kamati hiyo.
Wajumbe hao ni Marekani,China,Urusi,Cameroon,Uruguay Iceland Papua Guinea na Trinidad na Tobagona na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Prof. Kenedy Gaston amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu sana na ni ishara ya namna Tanzania inakubalika katika uso wa Jumuiya ya Kimataifa kutokana na uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli halikadhalika sera zake za mambo ya nje.
Balozi Prof. Kenedy Gaston ameongeza kuwa kwa mara ya kwana tangu uteuzi huo Tanzania imeongoza kikao chake cha kwanza cha kamati hiyo Kikao kilichofanyika New York,Marekani.
Post A Comment: