Sekretariet ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mkuranga Chini wa mwenyekiti wake Comrade Saidi King'eng'ena leo Jumatano tarehe 17/11/2020 imefanya kikao cha pamoja baina ya Makatibu wa CCM kata na Madiwani wa kata zote pamoja na madiwani wa viti Maalum kwa ajili ya kupeana maelekezo ya kazi za kiutendaji katika wilaya hiyo,
Vikao hivyo ambavyo sekretarieti ya Chama cha mapinduzi vimendelea kuwepo baada ya kumalizika Kwa Uchaguzi mkuu na hatimaye viongozi waliochaguliwa kupatikana na kilichobaki ni utendaji na maelekezo Kwa viongozi hao hasa makatibu wa CCM ambapo watarudi katika kata zao na kuendelea kujenga Chama cha mapinduzi sambamba na kushirikiana na madiwani katika kuwatumikia wananchi waliowapa dhamana.
Katika kikao hicho Katibu wa CCM Wilaya aliwakumbusha madiwani kuondoa tofauti zao kwa kuwa hazikisaidii Chama Chama Cha Mapinduzi, alisisitiza kuwa mahusiano mahusiano yapewe Kipaumbele katika kutimiza majukumu ya kila siku.
Post A Comment: