MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kufika kwenye ofisi za Tarura wilaya ya Tanga wakati wa
ziara yake |
MBUNGE
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akisistiza jambo kwa Meneja
wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene kushoto wakati wa
ziara yake |
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akionyeshwa maeneo mbalimbali kwenye mifereji wakati wa ziara yake na Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface MwambeneMBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wa pili kutoka kulia akitembelea maeneo mbalimbali wakati wa ziara yake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Mh Ummy Mwalimu ameanza kazi rasmi leo
za jimbo kwa kutembelea ujenzi na kukagua miradi ya barabara, mifereji
na madaraja ya kata nne ambazo ni Mnyanjani, Mabawa, Msambweni na
Ngamiani kati za halmashauri ya Jiji la Tanga ambazo zitagharimu kiasi
cha sh.bilioni 2.9.
Ummy alisema kuwa ameanza kazi kwani Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliahidi
na sasa kinatekeleza Ilani ikiwemo matengenezo ya barabara ya karume
mpaka machinjioni mita 600 ambayo itajengwa kwa kiwango cha changarawe,
barabara ya karume mpaka zahanati ya kwanjeka kwa kiwango cha
changarawe,
Huku akiitaja pia barabara ya 11 na 12 kuzunguka soko la Ngamiani itawekwa
lami,barabara ya Mabawa mpaka Msambweni ambayo itaongezwa lami yenye
urefu wa kilometa 2.
Aidha pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha Tarura ambazo
zitaenda kuboresha miundo mbinu ya barabara ndani ya Jimbo la Tanga
Mjini na kuwa kazi ndiyo zimeanza na hatakuwa mbunge wa ofisini bali
muda mwingi atakuwa ni wa kutembelea miradi na kutatua kero za wananchi
wa Tanga.
Naye Meneja wa
Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene amesema kuwa kwa
mwaka huu wa fedha wamesaini mikataba mitano ambapo ndani ya siku 14
wataanza kazi utekelezaji .
Miradi hiyo ipo
itayayotekelezwa kwa kiwango cha changarawe, lami ,ujenzi madaraja na
ukarabati wa mifereji ndani ya Jiji la Tanga barabara na amesema kuwa
watendelea kufanya kazi kama azma ya serikali ya hapa kazi tu.
kwa
upande wa madiwani akiwemo Yakub Nuru ambaye Diwani wa Mnyanjani wametoa
shukrani kwa mh. Ummy Mwalimu pamoja na serikali kupitia Rais Magufuli
kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Awali naye Diwani
wa Kata ya Mabawa, Athumani Babu alisema kuwa ilani ya chama cha
mapinduzi imeanza kutekelezwa kwani barabara ya kutoka komesho mpaka
chai bora yenye km 1 imeweka lami .
Hata hivyo kwa upande wake Diwani
wa kata ya Ngamiani Kati, Habibu Mpa ametoa shukrani zake kwa mh.
mbunge ummy mwalimu kwa kufuatilia ahadi ya waziri mkuu wakati
akifungua kampeni za Mbunge kuhusu kuweka lami barabara ya 11 na 12
yenye urefu wa mita 600.
Post A Comment: