Mshindi
wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani Wise Mgina akiwashukuru
viongozi wa chama pamoja na madiwani wote(hawapo pichani) kwa kumpa
nafasi ya kuwa kiongozi wa nafasi hiyo.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani Edward Haulge ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa kipindi kilichopita, akizungumza na madiwani wateule (hawapo pichani) baada ya uchaguzi kumalizika na kushindwa nafasi hiyo.
Madiwani wateule wa kata mbalimbali wilayani Ludewa wakiwa katika ukumbi wa CCM wilayani humo kumchagua mwenyekiti wa kamati ya madiwani.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, akizungumza na madiwani wateule (hawapo pichani) wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya madiwani uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya Ludewa.
Diwani mteule wa kata ya Mundindi Wise Mgina kushoto ambaye ndiye mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani akiwa na diwani mteule wa kata ya Ibumi Edward Haule ambeye ameshindwa nafasi hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere akizungumza kwa msisitizo na madiwani wateule (hawapo pichani) katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya madiwani uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya humo.
Diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu akitumbukiza karatasi ya kura katika sanduku kumchagua mwenyekiti wa kamati ya madiwani.
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume ( qliyesimama) akiwahesabia kura madiwani wateule waliogombea nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani Jimbo la Ludewa. Kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, mbele yao mweye shati la kijani ni mwenyekiti wa kamati ya madiwani aliyepita kwenye uchaguzi huo Wise Mgina na Edward Haule ambaye ameshindwa katika nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa vijana CCM wilaya ya Ludewa Theopista Mhagama (wakwanza kushoto) akizungumza na madiwani wateule pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa. Anayefuata ni Diwani mteule wa kata ya Ludewa Monica Mchiro, Diwani mteule wa kata ya Mawengi Leodgar Mpambalioto, Diwani mteule wa kata ya Ibumi ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani Edward Haule, Diwani mteule wa kata ya Mundindi ambeye ndiye mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani Wise Mgina na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga.
Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na madiwani wa kata zote za
jimbo hilo wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta Maendeleo
katika jimbo hilo.
Hayo ameyasema katibu wa CCM wilaya ya Ludewa
Bakari Mfaume wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa kamati ya madiwani
uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilayani humo.
Katibu huyo
amesema kuwa umoja wao ndio nguzo pekee ya maendeleo na itawasaidia
kutekeleza kwa urahisi miradi mbalimbali iliyomo ndani ya ilani ya
chama.
Katika uchaguzi huo ambao ulihudhuliwa na Mkuu wa wilaya
hiyo Andrea Tsere, Mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga, Mwenyekiti wa
CCM wilaya Stanley Kolimba, madiwani wa CCM wa kata 23 pamoja na
madiwani 8 wa viti maalum pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya wilaya.
Wagombea
wa nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya madiwani iliyogombewa na watu
wawili ambao ni Diwani mteule wa kata ya Mundindi Wise Mgina pamoja na
Diwani mteule wa kata ya Ibumi Edward Haule ambaye ndiye aliyekuwa
anashikilia nafasi hiyo kipindi kilichopita.
Katika uchaguzi huo Wise Mgina amepata ushindi wa kura 19 na kupelekea mpinzani wake kupata kura 13 Kati ya kura 32 zilizopigwa.
Akizungumza
baada ya ushindi huo Mgina amesema atafanya kazi bila ubaguzi wowote
hivyo ameomba madiwani wote kumuunga mkono katika harakati za kuleta
Maendeleo wilayani Humo.
Aliongeza kwa kuwaomba wakazi wa Ludewa
hasa kwenye makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii kuangalia uchaguzi
wa Sasa badala ya kuzungumzia uchaguzi wa 2025.
Alisema kwa sasa
wanapaswa kushirikiana na viongozi waliopita kusukuma gurudumu la
Maendeleo na si kuanza kuwajadili viongozi walioingia madarakani.
"
Watu wanajadili juu ya uchaguzi ujao ambao kwa sasa hauna tija yoyote!
Mnapaswa kutupima kwa utendaji wetu ndipo mtujadili na si kuanza
kujadili watu kabla hata hawajaanza shughuli za utekelezaji", Alisema
Mgina.
Naye Haule amewashukuru wote kwa kukamilisha mchakato huu na kuahidi kuonyesha ushirikiano mzuri kwa mwenyekiti aliyepita.
Aidha
kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga amewataka madiwani
hao wateule kumuhusisha katika changamoto mbalimbali zinazowasilishwa
kwao kutoka kwa wananchi ili kuweza kuzitatua na kuzijadili kwa pamoja.
"Tufanye
kazi kwa pamoja, mimi siko upande wa mtu yeyote! Bali nahusiana na watu
wote kikubwa ni kuleta Maendeleo ndani ya Ludewa".
Post A Comment: